Saturday 23rd, November 2024
@Wilaya ya Longido
Wilaya ya Longido imepatiwa kiasi cha tani 40 za mbolea ya kupandia, tani 40 za mbolea ya kukuzi na tani 8 za mbegu za mahindi kwa ajili ya wakulima 800 katika mfumo wa pembejeo zenye ruzuku ya serikali katika msimu wa kilimo wa 2016/2017. Aidha,kikao cha kamati ya pembejeo ya wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya longido tarehe 16/01/2017 kilipitisha mgao na kupanga bei elekezi za kuuza pembejeo hizo katika vituo ambavyo ni makao makuu ya kila Kata ambazo zitapatiwa pembejeo. Sambamba na hilo Mawakala Wiana Agrovet na Atau Agrovet watahusika na usambazaji wa pembejeo katika Wilaya ya Longido kwa msimu wa kilimo wa 2016/2017.
Kwa msimu wa Kilimo 2016/2017 baadhi ya Vijiji ikiwemo vijiji vya Tingatinga, Sokon, Ngereyani, Mundarara, Mairowa vitakosa Pembejeo yenye ruzuku kwa sababu Wilaya imepatiwa kiasi kidogo cha pembejeo tofauti na misimu iliyopita, hivyo vijiji na wakulima wachache (wakulima 800) ndio watakaopatiwa pembejeo hali itakayopelekea wakulima wengi kukosa pembejeo hizo zenye ruzuku. Bofya hapa kuona mgao kwa vijiji.Mgao wa Pembejeo.doc
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM