Suala la ajira mpya katika Utumishi wa Umma hufuata misingi ya mahitaji halisi ya rasilimali watu na upatikanaji wa rasilimali fedha. Ajira mpya haziwezi kufanyika pasipo kuwepo kwa uhitaji ulioainishwa rasmi pamoja na bajeti iliyoidhinishwa (Ikama).
Mahitaji Halisi ya Mtumishi Mpya:
Mwajiri anawajibika kubaini maeneo yenye upungufu wa watumishi kwa kuzingatia ufanisi wa utoaji huduma. Uhitaji huu huainishwa katika mipango ya rasilimali watu ya taasisi husika.
Upangaji wa Bajeti (Ikama):
Kabla ya kujaza nafasi yoyote mpya, taasisi lazima itenge fedha kwenye bajeti kwa ajili ya kugharamia mishahara na stahiki nyingine za mtumishi atakayejiriwa.
Jukumu la Mwajiri:
Ni wajibu wa mwajiri kutathmini na kuwasilisha taarifa ya uhitaji wa watumishi kwenye ngazi husika kwa ajili ya kuridhiwa na kuidhinishwa, sambamba na kuandaa bajeti ya ajira hizo.(OFISI YA RAISI MENEJIMENTI YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA )
Upatikanaji wa Kibali cha Ajira:
Kama ilivyo kwa ajira mbadala, ajira mpya pia haziruhusiwi bila kupata kibali cha ajira kutoka kwa mamlaka husika. Kibali hiki hutolewa kwa kuzingatia:
Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 1999
Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, pamoja na marekebisho yake Na. 17 ya mwaka 2007
Uzingatiaji wa Taratibu za Ajira:
Taratibu zote za ajira ni lazima zizingatie sheria, kanuni, miongozo na taratibu za ajira za umma, ikiwa ni pamoja na uwazi, ushindani wa haki, na vigezo vya sifa za nafasi husika.
Tembelea Tovuti:
KWA MAWASILANO ZAIDI TUPIGIE
0717022718 Afisa Utumishi wilaya ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.