Baraza la madiwani la halmashauri ya Longido limeitaka TARURA kurekebisha miundombinu ya barabara iliyoharibiwa vibaya na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
Hayo yamesemwa leo tarehe 2/5/2018 na baraza hilo wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kata kwa robo ya tatu kuanzia januari mpaka machi 2018 mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri.
Aidha madiwani wa kata 17 wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa za kata zao huku taarifa hizo zikionyesha shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata, Elimu,Afya, Maji, Miundombinu ya barabara, pamoja na taarifa za ulinzi na usalama na changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Jumaa Mhina akichangia katika baraza hilo alisema kuwa,Halmashauri imepewa jukum la kuibua barabara na kuhoji kiwango cha ubora wake na TARURA ndio wenye mamlaka ya kuamua namna ujenzi huo utakavyoendelea.
Naye katibu tawala wilaya ndg.Toba Nguvila akichangia changamoto kubwa ya uharibifu wa miundombinu iliyowasilishwa na wajumbe wa baraza, alisema, TARURA ni taasisi ambayo ipo chini ya Mkuu wa Wilaya na kwa sasa inafanya kazi kwa bajeti ya 2017/2018 hivyo basi kama Uongozi wa Wilaya watajitahidi waweke mahusiano mazuri kati ya TARURA na Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Sabore Molloimet aliitimisha mkutano huo kwa kusema taatifa hizo zimepokelewa na hivyo kusimamiwa katika suala zima la utekelezaji.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM