Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Longido leo tarehe 25/01/2019 limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya kiasi cha Tsh.23,384,205,100/- ikiwa ni matumizi na makusanyo kutoka vyanzo vifuatavyo; Mapato ya ndani ,Ruzuku ya Mishahara ,Ruzuku ya matumizi mengineyo na Ruzuku ya miradi ya Maendeleo .
Bajeti hiyo imewasilishwa na Afisa Mipango, Wakuu wa idara na Wakuu wa vitengo , Hivyo basi wajumbe wa Baraza walipata fursa ya kuijadili rasimu hiyo ya bajeti na kuipitisha.
Kikao hiki cha Baraza la Wafanyakazi kupitia na kujadili rasimu ya bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019 /2020 ni mwanzo wa vikao vya kamati mbalimbali pia kujadili makisio hayo ya bajeti kwa mwaka 2019/2020.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM