Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Frank Mwaisumbe leo tarehe 17.04 .2020 amepokea msaada wa mafuta ya diesel lita 250 yenyewe thamani ya Tshs 530,000/= kutoka kwa Chama cha Ushirika cha Usafirishaji cha KIMANA na Umoja wa Madereva wa magari ya abiria aina ya Noah zinazofanya Safari kati ya Namanga na Arusha. Mafuta hayo yametolewa ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika Wilaya ya Longido kukabiliana na kuenea kwa virusi vya COVID -19 na yatatumika kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa Elimu kwa Umma zoezi litakaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Akipokea msaada huo katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya Longido Mhe Mwaisumbe aliupongeza umoja huo kwa kutambua juhudi za Serikali na kuwataka kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha janga la corona linatokomezwa. Alisema sekta ya usafirishaji ina jukumu muhimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wasafiri wananawa mikono kabla ya kupanda magari na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale watakapoona kuna mtu mwenye dalili za ugonjwa huo. Pia aliwataka kutoa ushirikiano kwa kuwaripoti kwenye mamlaka husika wasafiri ambao wanatumia njia zisizo rasmi katika mpaka wa Namanga kuingia Nchini bila kupimwa Afya zao hivyo kutishia kuongezeka kwa maambukizi na wahamiaji haramu. Pamoja na hayo Mhe Mwaisumbe alitoa wito kwa wadau wengine na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa michango kwa Mfuko wa Maafa wa Taifa ili kuwezesha Serikali kukabiliana na corona.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na baadhi ya wajumbe wa KIMANA SACCOS wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ndg Rashid Masoud na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji iliwakilishwa na Ndg Edward Kasiga na Afisa Ushirika Ndg Gabriel Mambo
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM