Asilimia 95% ya wananchi wa wilaya ya longido ni wafugaji wa ngombe ,mbuzi,kondoo na punda,mbwa,ngamia,kuku na nguruwe.
Idadi ya mifugo katika wilaya ya Longido ni Ng’ombe 216,575, Mbuzi 399,754, kondoo 301,211 na punda 7,14,Ngamia 240,mbwa 15,032 na Nguruwe 965.
Katika kuuthibiti ugonjwa wa kimeta(anthroux) ambao umebainika kuwepo mnamo tarehe 25/01.2019 baada ya kupokea taarifa ya kifo cha mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 11 kilichotekea baada ya kula nyama ya ngombe aliyekufa akisadikika kuwa na ugonjwa wa kimeta,baada ya uchunguzi iligundulika ni kweli ngombe huyo alikuwa na kimeta .
Tarehe 28/02/2019 Serikali makini ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel ilitoa kwa Halmashauri dose 35,000 za chanjo ya kimeta, ambazo aliagiza kuwa zitolewe bure ambapo kila ng’ombe atakaye chanjwa alipiwe Tshs. 200/=@ badala ya 400/=@ inayotozwa sasa na Tshs. 100/=@ kwa kila mbuzi/kondoo atakaye chanjwa badala ya Tshs. 300/= inayotozwa sasa kwa mbuzi/kondoo kwa sasa. Aidha alielekeza chanjo hizo zitumike bila kuathiri mpango wa uchanjaji wa Wilaya uliowekwa.
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido alitoa pesa za kununua chanjo za ugonjwa huo, ambazo ni chupa 100 sawa na dozi 10,000 yenye thamani ya Tshs. 2,000,000/= (Revolving money). Lengo ikiwa ni kuchanja mifugo yote ya Wilaya nzima. Chanjo hiyo tumeshaanza kuitumia kuchanja mifugo kwa bei ya Tsh. 400/= kwa ng’ombe na mbuzi/kondoo Tshs. 300/=. Halmashauri imeweza kununua vitendea kazi ili kurahisisha uchanjaji wa ugonjwa wa kimeta mapema na kwa wakati.
Hadi kufikia tarehe 05/03/2019 jumla ya ng’ombe 4850 na mbuzi/kondoo 5785 walishachanjwa katika vijiji vya Tingatinga, Ngereyani na Orbomba na zoezi hili ni endelevu.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM