HALMASHAURI YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI.
Halmashauri ya wilaya ya longido Leo tarehe 15/11/2017 imetoa mkopo wa fedha za kitanzania sh.16,700,000/- kwa vikundi vinne vya kina mama na vijana.
Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Nd.Lotta wakati wa sherehe za makabidhiano hayo amesema vikundi hivyo ni vya bodaboda ,wakulima, mifugo na kikundi cha ushonaji wa shanga na urembo wa kimasai.
Pia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Nd. Jumaa Mhina wakati wa makabidhiano hayo amesema pesa hizo zinazotolewa za mikopo ni za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido na mkopo unatolewa bila riba yoyote kwa vikundi vyote ikiwa ni kutekeleza agizo la Mh Rais la kutoa asilimia 5% kwa vijana na asilimia 5% kwa wanawake.
Akikabidhi mikopo hiyo mgeni rasmi ambaye ni Katibu tawala Wilaya Nd.Toba Nguvila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Longido ,amewaasa wanavikundi kuwa pesa zinazotolewa Leo ni kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza kipato cha wanavikundi na si kwa matumizi mengine.
Vile vile vikundi vilivyopata mikopo wametoa shukrani zao za dhati kwa Halmashauri ya Longido na kuahidi kutumia mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM