Halmashauri ya wilaya ya longido leo tarehe 12/04/2019 yaaendelea kunufaisha vikundi mbalimbali vya halmashauri kwa kuvipatia mkopo usio na riba.Jumla ya vikundi 14 vimenufaika na mkopo unaotolewa na halmashauri kila baada ya miezi minne/kila robo ya mwaka ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali la kutaka kila halmashauri kutenga asilimia 10% ya mapato ya ndani ya halmshuri kwa ajili ya vikundi mbalimbali.
vikundi vilivyo nufaika na mkopo huo ni
1 Namayana - noondoto
2 Nailepwa - mairowa
3 Namayana b-leremeta
4 Enaiboshu -ildonyo
5 Tunawajali -longido
6 sayuni longido
7 naiba osina -irkaswa
8 Iloonyok - engikaret
9 Noondishu -Eworendeke
10 The great queen Longido
11 Tuwepa longido
12 Tumaini Osiligi Eworendeke
13 Kimawalo Longido
14 Wema -Lerang'wa
Akizungumza katika hafla hiyo Ndg.Nestrory Dagharo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ,amesema Vikundi 14 vimepata mkopo wa jumla ya shilingi millioni 40 na hadi sasa tumeshatoa zaidi ya shilingi million 131 kwa ajili ya vikundi mbalimbali vya halmashauri ya wilaya yetu ,Nawasihi mkatumie kwa jinsi mlivyo ainisha kwenye shughuli zenu bila kuathiri malengo ya vikundi vyenu .
"Vile vile halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vingine mbalimbali katika halmashuri yetu hivyo basi nawasihi mkafanye kazi na mrudishe mkopo kwa wakati ili na vikundi vingine viendelee kunufaika"alisema kaimu mkurugenzi Nestory.
Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Madiwani , Mh.Witness amewaasa wanavikundi kutumia fursa hii vizuri wa ajili ya kuleta maendeleo na kubadilisha hali yao ya maisha .
Mkaone kwamba Mungu amewatendea miujiza ,wilaya ina vikundi vingi sana nyie mliopata nafasi hii mkapate kutumia na kurudisha fedha hii kwa wakati ili na vikundi vingine vipate kunufaika na mkopo huu.msiende kutapanya pesa kwenye njia ambayo sio sahihi kwani hata sisi viongozi wenu tunawafuatili hatua kwa hatua ili fedha hizi ziweze kurudi kwa wakati na kukopeshwa vikundi vingine.
Nae afisa maendeleo ya jamii wilaya ya longido Grace Mghase amesema mpaka sasa halmashauri imetoa millioni 16 kwa ajili ya walemavu ni jambo zuri kuona kwamba vikundi vya walemavu vinaongezeka kwani wamekuwa wakifichwa majumbani kitu kilichokuwa kinawaathiri walemavu wengi na kukosa msaada kwa serikali hasa katika maeneop haya kifugaji ,Fedha hizi zikatumike kwa ajili ya kuboresha na kuinua uchumi wenu wanakikundi alisema Grace.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM