Mwenyekiti wa CCM Mkoa ndugu Steven Zelote pamoja na kamati ya Siasa mkoa wa Arusha wamefanya ziara wilayani Longido tarehe 22/03/2023 ambapo wametembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo Wilayani humo
Miradi iliyotembelewa ni kama ujenzi wa madarasa katika shule ya Engong'osunyai katika kijiji cha Ngereyani kata ya Tingatinga, ikiwa ni ujenzi wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo, pia kamati ya siasa mkoa wa Arusha imetembelea ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari ya Tingatinga ambalo limegharimu fedha takribani milioni arobaini za kitanzania bweni hilo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 120 kwa mkupuo mmoja, na liko katika hatua za mwisho za kukamilika ili kuanza kutumika, bweni hilo la wavulana linataraji kukamilika na kukabidhiwa mnamo mwishoni mwa mwezi wa tatu vile vile kamati imekagua ujenzi wa Maktaba ambao mradi ulisainiwa tarehe 14 Juni 2022 mradi huo wa ujenzi wa maktaba umegharimu kiasi cha shilingi milion 62 kati ya hizo fedha kiasi cha shilingi milioni 52 zimetolewa na wafadhili wa mradi PROBONO na kiasi cha shilingi milioni 10 imetolewa na Halmashauri na kufanya ujenzi huo kutumia kiasi cha shilingi milioni 62 ili kumalika, ikiwa bado lina upungufu wa shelf za kuhifadhia vitabu na meza kwa ajili ya wananfunzi.
Naye mkuu wa shule Mr Palanjo ameiomba kamati ya siasa pamoja na serikali kwa ujumla kutengeneza uzio katika shule hiyo ili kuzuia uvamizi wa wanyama hususani tembo kwakuwa wamekuwa tishio kwenye shule hiyo, sambamba na hilo mkuu wa shule ameiomba serikali kumaliza tatizo la maji shuleni hapo kwani ndio changamoto kubwa inayosumbua shuleni hapo ukizingatia shule hiyo ni ya bweni na ina wanafunzi wengi, maji yaliyopo hayatoshi na hayo machache wanachi wa vijiji vingine wamekuwa wakipasua mabomba kwa ajili ya mifugo kabla hayajafika shuleni hapo
Pia kamati imetembelea ujenzi wa hospital ya wilaya ya Longido ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilika na tayari hospitali hiyo imepokea vifaa tiba mbali mbali kama vile mashine ya mionzi yaani X ray, utra saund pamoja na vipimo vingine aidha mwenyekiti wa kamati ya siasa ameuomba uongozi wa wilaya ya Longido kuongeza kasi katika ujenzi huo ili wananchi wapate huduma bora na kwa haraka
Pia kamati imepita katika shule ya sekondari ya Longido na kukagua ujenzi wa madarasa pamoja na ofisi ya walimu vile vile ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Longido ambalo nalo liko katika hatua za mwisho kukamilika.
Kamati ya siasa imehitimisha ziara yake katika mradi wa maji Namanga ambao umekuwa ukiwasambazia maji wananchi wa namanga na vitongoji vyake pamoja na uchache wa maji katika mradi huo wataalamu wa maji Auwasa wameimbia kamati kuwa wamepanga utaratibu wa kuchimba kisima kirefu kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo na kwa kuwa ni mradi mkubwa usaidia sana kuondoa changamoto ya maji ndani na nje ya Namanga.
Naye mkuu wa wilaya ya Longido mheshimiwa Marko Ng'umbi ameishukuru sana kamati ya siasa ya mkoa kwa kufanya Ziara katika miradi ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kusimamia vema na kwa uadilifu mkubwa ili iweze kumalika kwa wakati na kutumika kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Longido na vitongoji vyake sambamba na hilo pia amemshukuru Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi mbali mbali kwenye halmashauri ikiwemo madarasa, mabweni, vyoo, pamoja na hospital na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo ya mkoa.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa John Mongela amepongeza uongozi wa Halmasahauri ya walaya ya Longido kwa kazi nzuri kwani miradi yote iliyo tembelewa ni mizuri inaendelea vizuri, imesimamiwa vema na imeendana na thamani ya pesa iliyotumika ama kutolewa na serikali ya awamu ya Sita
Aidha mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa ndugu Steven Amewaomba wanachama wa ccm pamoja na wataalamu kufuata kanuni na taratibu za na pia kufuata muongozo wa katiba ya chama cha mapinduzi ikiwa moja ya ilani za chama ni kusimamia ukamilishwaji wa miradi inayotolewa na serikali kwenda kwa wananchi
Vile vile mwenyekiti wa CCM mkoa amewaasa wana Longido kuwa makini na utumiaji sahihi wa mitandao kwani matumizi yasio sahihi uleta uchochezi kwa jamii "Ndugu zangu wana Longido tujitahidi kumaliza changamoto zenu wenyewe bila kushirikisha mtu wa pembeni na iwapo itatulazimu kufanya ivyo basi tufuate utaratibu kanuni na sheria kwa sababu sheria zipo na ziko wazi" Alisema ndugu Steven Zelote
Aidha Mwenyekiti huyo wa chama amemshukuru mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbali mbali yenye tija kwa wananchi "Kusimamia miradi vizuri na kukamilisha kwa muda uliopangwa itamsaidia Rais wetu kutuongezea fedha kwa miradi mingine mizuri yenya tija kwa wananchi kama barabara shule masoko pamoja na miundo mbinu mingine" alisema Stiven Zelote. Aidha amemaliza kwa kuwataka wanachama kufanya kazi kwa kushirikiana bila kuoneana ikiwa na lengo la kumuunga mkono mama Samia na kusongesha gurudumu la maendeleo na kutimiza ilani za chama cha Mapinduzi.
*Jamhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM