Leo tarehe 06-10-2021 kamati ya Siasa wilayani Longido imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi iliyoko katika kata ya Sinya na Tingatinga ikiwemo Bwawa la Mifugo,kituo cha mawasiliano, ujenzi wa jingo la utawala na maabara ya Komputa katika shule sekondari Tingatinga na mradi wa Mizinga ya nyuki katika kata ya Tingatinga.
Katika ziara hiyo Katibu wa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Enduiment (EWMA) wilayani Longido Mkoa wa Arusha Igno Laitayok amesema walipokea fedha shilingi billion 1.9 kutoka kwa Mfuko wa wanyamapori duniani (WWF) kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF)katika jumuiya hiyo.
Akielezea miradi iliyotekelezwa kwa kamati ya Siasa ya wilaya (CCM) alisema miradi hiyo ililenga kubabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi pamoja na kudhibiti migongano baina ya wanyamapori na binadamu,ikiwemo ujenzi wa bwawa Endemwa lenye gharama ya shilingi million 106.
Alisema ujenzi wa bwawa katika mpaka wa kata ya Sinya na Olmolog utasaidia kupatikana kwa maji kwa mifugo na wanyamapori,na mradi huo umewekewa uzio ili mifugo wasiweze kuingia na kuharibu miundombinu lakini Kuna birika(cattletraff) kwa ajili ya kunyweshea mifugo na wanyama katika eneo la bwawa.
" Uwepo wa bwawa hili utapunguza migogoro baina ya wanyamapori na binadamu nyakati za utafutaji wa maji" alisema Laitayok.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Joseph Ole Sadira alipongeza na kuwashukuru wadau hao ,huku akitoa wito kwa halmashauri kuwapa ushirikiano wadau hao wakati wa utekelezaji wa miradi kwa manufaa ya jamii,hususani wataalamu wa Halmashauri hiyo.
" Miradi ya wafadhili ni mizuri kweli ,na hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zao na ufuatiliaji,huko Kwa wafadhili hakuna wizi Wala ubadhirifu" alisema Ole Sadira.
Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Zakaria Faustin alisema wametekeleza miradi maeneo mbalimbali ikiwemo WMA ya Ikona huko Meatu ,lakini eneo lililopata miradi ya upendeleo ni EWMA,na halmashauri iliwapa ushirikiano wa kutosha.
" Hapa tumewapa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa ofisi ya jumuiya shilingi millioni 427,000,000,Ujenzi wa kituo Cha utoaji wa taarifa za utali shillingi millioni 225,000,000 na kujenga kituo Cha Hali ya hewa shilingi millioni 20,000,000 hiyo ni mifano ya miradi" alisema Faustin.
Mkurugenzi mtendaji Ndg Stephen Ulaya naye aliwashukuru Wadau hao kwani wameisaidia serikali kutekeleza mahitaji ya jamii “kwani kimsingi sisi serikali tulitakiwa kutekeleza haya hivyo basi fedha kidogo iliyotakiwa kuletwa kutekeleza mradi huu utaelekezwa sehemu nyingine kutatua changamoto za jamii yetu”.
Aidha , Mwenyekiti wa Halmashauri Simon Oitesoi alisema wafadhili hao wametekeleza majukumu ya halmashauri hiyo,na kuwaomba wasiishie hapo waendelee kusaidia serikali katika kutekeleza mahitaji ya wananchi.
Naye Mkuu wa Wilaya Nurudin Babu alisema wilaya hiyo ni ya kifugaji na uhifadhi hivyo miradi hiyo imelenga uhalisia wa eneo husika,na kueleza kuwa uwepo wa bwawa litasaidia kuondoa mwingiliano baina ya wanyamapori na binadamu katika makazi.
" Wanyama wakipata maji hapa hawataweza kwenda kwenye jamii kuleta taharuki kwani huduma zao zimesogezwa karibu na mazingira Yao"
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM