• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

KAMATI YAKOSHWA NA UJENZI WA MADARASA TINGA TINGA SEKONDARI.

Posted on: February 27th, 2019

Kamati ya Fedha na Mipango Halmashauri ya Longido leo tarehe 27/02/2019 imehitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo  kumi na tano (15) kwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019  ikiwa ni utaratibu wa kisheria kwa kamati hii kutembelea miradi kwa kila robo.

Kamati imetembelea ujenzi wa madarasa manne  shule ya sekondari Tinga Tinga ,Ujenzi wa madarasa shule ya msingi Tinga Tinga,Ujenzi wa mabweni na madarasa shule ya sekondari Enduimet,Ujenzi wa kituo cha afya Ketumbeine,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Ketumbeine,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Flamingo,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Lekule sekondari,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Namanga,Ujenzi wa hospitali ya Wilaya.Ujenzi,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Namanga,Ujenzi wa madarasa shule ya msingi Orbomba,Mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Oltepes,Ujenzi wa madarasa Sekondari ya Engarenaibor,Ukamilishaji wa Ujenzi sekondari ya Matale, na ujenzi wa kituo cha Afya Engarenaibor.

Wajumbe wa kamati hiyo wametoa maagizo mbalimbali kwa miradi waliyokagua lakini wameridhishwa zaidi na ujenzi wa madarasa manne ya shule ya sekondari Tinga Tinga ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi kuanzia msingi mpaka kufikia hatua ya umaliziaji yakiwa na kiwango cha juu na gharama ndogo. 

Nao wananchi wa Tinga Tinga wameiomba serikali iwaangalie kwa jicho la pekee kwani hatua waliyofikia wanaomba washikwe mkono ukizingatia kwa sasa wana miradi mingine wanayotekeleza kwa nguvu za wananchi ikiwa ni mradi wa Zahanati na madarasa ya shule ya msingi yote yanajengwa kwa nguvu za wananchi.

Mh Diwani Naomi Mollel amewapongeza sana wananchi wa Tinga Tinga kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuwataka waendelee na moyo huo wa kuchagia miradi ya maendeleo, "Hakika juhudi yenu wanachi wa kata ya  Tinga Tinga  ya kuchangia miradi ya maendeleo ni kubwa sana kuliko kata yoyote katika halmashauri yetu,niwapongeze kwa hilo na sisi kama wajumbe wa kamati ya Fedha tunalibeba hili na kuliwasilisha katika kikao cha kamati ya Fedha kitakochokaa keshokutwa ili tuone namna gani tutawashika mkono ingawa kama Halmashauri tuna miradi mingi kila mahali lakini haiwezekani kwa juhudi zenu hizi tuwaache hivi hivi" alisema Mh.Naomi Mollel.

Nae Mh.  Kenedy Sabore ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido akizugumza na baadhi ya wanakamati katika shule sekondari Engarenaibor amefurahishwa na mwamko wa wananchi kuchangia maendeleo ya kata zao ambapo kata ya Engarenaibor wamechangia madarasa mawili na ofisi moja na kata ya Mundarara wamechangia madarasa mawili na ofisi moja jumla madarasa manne na ofisi moja ambazo zote zipo hatua ya lenta."Ndugu wanakamati hongereni sana kwa kazi nzuri ya ujenzi wa madarasa katika kata zenu tunatambua umuhimu wa michango yenu katika uharakishwaji wa maendeleo ya kata zenu na wilaya kwa ujumla,ombi langu endeleeni na moyo huo huo wa kujitolea kwa ajili maendeleo ya wilaya yetu,pili kamati ya ujenzi mjitahidi kuwalinganisha mafundi wazoefu na wa bei nafuu ili kuweza kufikia malengo ya gharama iliyopo kwenye makisio ya mhandisi (BOQ)  "alisema Sabore".

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA UMMA April 12, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA May 15, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA June 25, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • View All

Video

MKUU WA WILAYA YA LONGIDO AUNGANA NA RC KIHONGOSI KWENYE JOGGING YA TANZANIA SAMIA CONNECT
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.