Kamati za maji za miradi ya Tabia nchi kutoka katika vijiji vya Kiserian,Orbomba,Eorendeke,na Namanga zimepatiwa mafunzo ya jinsi ya kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe endelevu na kuwaletea maendeleo kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 01-02/2018
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa elimu sekondari(W) Mwalimu Gerson Mtera amezitaka kamati hizo kuilinda na kusimamia miradi hiyo kwa kuwa wao wenyewe ndiyo waliibua miradi hiyo na ikapitishwa na ikapata wafadhili na kutekelezwa pindi watakapokabidhiwa ni jukumu lao kuitunza ili iwe endelevu na kuwaletea maendeleo katika vijiji vyao.
Pia mratibu wa miradi ya Tabia nchi ndg. Ally Msangi nae amezitaka kamati za maji kuwa wasimamizi wakuu wa miradi hiyo pindi itakapo kabidhiwa ili miradi yao iwe endelevu na yenye tija na mada zifuatazo ziliwasilishwa kwa wanakamati:-
- Nini maana ya mabadiliko ya Tabia nchi,
-uendelevu wa miradi
-ushirikishwaji wa jamii katika miradi
-uwakilishi sawa katika kamati za maji
-Uandaaji wa bajeti ya uendeshaji na ukarabati
-Utawala na usimamizi bora wa miradi
-Uandaaji wa taarifa za miradi na utunzaji kumbukumbu
-Tadhiminii na ufuatiliaji wa miradi.
Kwa upande wao wajumbe wa kamati hizo wamesema wameelewa vizuri mafunzo hayo na wanashukuru kwa kuwa nii Mara ya kwanza kwa kamati hizi kupatiwa mafunzo na wamehaidi kuitunza miradi hiyo kwa nguvu zao zote.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM