Katibu tawala mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia leo tarehe 17-11-2021 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Afya na Elimu iliyopokea fedha za Mpango wa serikali ya Tanzania wa kuinua Uchumi kwa kutumia mkopo wa fedha wa Sh. Trillion 1.3 uliotolewa na shirika la fedha Duniani (IMF) na kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO 19) ili kuangalia utelezaji wa miradi hiyo wilayani Longido.
Katibu TawalaMkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia amesema wilaya ya Longido ni moja ya wilayailiyopewa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi kutokana naJiografia ya eneo hilo,na kutoa wito kwa wasimamizi wa ujenzi kutofanyaubadhirifu wa fedha hizo.Dkt Kihamia alisema wilaya hiyo imepewa sh billion 1kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa 50 maeneo mbalimbali katika wilaya,fedha hizini za moto msijaribu kuzitumia kinyume na kile kilichoagizwa.
Akizungumzia hali ya miradi inavyotekelezwa ,alisema pamoja na kuwa wilaya hiyoupatikanaji wa Nyenzo(Material) kwa ajili ya ujenzi ni changamoto lakini viongoziwamejitahidi kusimamia tofauti na maeneo mengine ambayo malighafi yanapatikanakwa haraka." Mmejitahidi na mpo kwenye hatua nzuri,lakini haimaanishi kuwammeshamaliza kazi bado,tutarudi kukagua na wataendelea kuja watu kutoka maeneombalimbali kwa ajili ya kukagua miradi hii ikiwemo TAKUKURU"Alisema DktKihamia.
Katika hatua nyingine,aliwahasa wazazi kuwapeleka watoto shule na kuachana nadesturi ya kuwachungisha mifugo,kwani serikali inatambua haki ya elimu kwamtoto ndio maana Rais Samia ametoa fedha za ujenzi wa Madarasa hayo nakuwasogezea huduma karibu watoto wasiendelee kutembea umbali mrefu kufuataelimu.
Jacob Laizer Mkazi wa Kata ya Orbomba Tarafa ya Longido akizungumza kwa niabaya wananchi alitoa shukrani kwa Rais Samia kwa kuleta fedha za miradi ya elimuna kudai kuwa shule nyingi wilayani humo zenye ufaulu duni wa watoto nikutokana na umbali mrefu wa kwenda shule.Alisema,uwepo wa shule hizo karibu najamii kutasaidia kupunguza kwa kuzorota kwa elimu kwa watoto wa jamii yakifugaji,kwani Uvivu wa kutembea zaidi ya kilomita 10_25 kufuata elimuutapungua na watoto watasoma kwa raha." Hata hivyo watoto wetu walipokuawakitembea umbali mrefu kufuata elimu kwenye shule mama za msingi walikuawakikutana na wanyama wakali Hali hiyo pia ilikua ikiwatia hofu na kukata tamaaya kuendelea na masomo na kupeleka utoro sugu wa wanafunzi" alidai Laizer.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Nurudin Babu katika ziara yake aliwasisitiza jamiihiyo kutumia majengo hayo pindi yatakapo kamilika kwa kuhakikisha watotowanakwenda shule ili yasibaki Kama Ghofu na nyumba ya wadadu Kama vile Buibui.Aidha aliwataka jamii kujiongeza kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika maeneoyaliyojengwa shule shikizi sambamba na Madarasa hayo ili watoto watakapoanzakusoma wapate huduma ya vyoo na kuepuka kujisaidia maeneo yasiyorasmi Mfanovichakani." Naomba acheni tabia ya kuwakeketa watoto wakike pamoja na ndoaza utotoni" aliomba Babu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Stephen Ulaya alisema pamojana kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maji na matofali,lakini wamejipangakukabiliana nalo na ifikapo Desemba 15 Madarasa hayo yatakua yamekamilika.
Ikumbukwe kuwa fedha hizi ni fedha za Mpango wa serikali ya Tanzania wa kuinuaUchumi kwa kutumia mkopo wa fedha wa Sh. Trillion 1.3 uliotolewa na shirika lafedha Duniani (IMF) na kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO 19).
Mafundi ujenzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na RAS katika ujenzi wa vyumba vinne shule shikizi Odorko.
Ujenzi wa madarasa mawili ya shule sekondari ya Namanga
Ujenzi wa madarasa mawili ya Sekondari ya Longido
Ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa Katika shule ya Sekondari Engarenaibor
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM