Kikao kazi cha bajeti na fedha kinachoendelea kufanyika katika halimashauri ya wilaya ya longido ambacho kinajumuisha idara zote za halmashauri katika kupanga bajeti ya fedha ya mwaka2018
Akifafanua zaidi kaimu afisa mipango na bajeti NDg.Peter Ngussa amesema kuwa kikao cha bajeti na fedha kinahusisha idara zote za halmashauri na kusema zoezi hilo la bajeti bado linaendelea.
Pia ameeleza kuwa ni kila mwaka vikao vya bajeti hufanyika na kila idara inaandaa bajeti yake na kila idara inaingiza bajeti yake mwenyewe Kwenye mfumo wa planrep wa bajeti hivyo nilazima kuwa na akaunti na minwila kwa Mkuu wa idara pamoja na msaidizi wake.
Vilevile ngussa aliendelea kufafanua kuwa kwa kila mwaka huwa wanaandaa bajeti na katika bajeti hiyo kunakuwa na bajeti ya maendeleo na bajeti ya kawaida
Hata hivyo ameeleza kuwa kila bajeti ya mwaka inayoandaliwa inatofautiana na bajeti ya miaka mingine hii ni kutokana na mapato ya ndani na mapato ya serikali ambayo yanategemea ukusanyaji wa bajeti ya kila mwaka.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM