"Ni jukumu la kila mmoja wetu kuzingatia na kufuata taratibu na kanuni bora za lishe kwa Afya ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla "Alisema Ndugu Stephen A. Ulaya alipokuwa akifungua kikao cha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwezi Julai hadi Septemba 2023, katika Ukumbi wa J. K Nyerere leo tarehe 6/11/2023
Akisoma taarifa ya Lishe ya wilaya Ndugu Daniel Mwenda kwa niaba ya Afisa Lishe wilaya taarifa inaonesha hali ya Lishe kwa kaya na wananchi waishio Longido ambako ilionyesha 85.98% ya watoto chini ya umri wa miaka mitano wana hali nzuri ya lishe na 13.40% wana utapiamlo wa wastani na 0.61% wana utapiamlo mkali. Hivyo basi kutokana na tathmini hii kiwango cha utapiamlo mkali kimepungua kwa asilimia 0.11% kutoka asilimia 0.72% ya robo ya Aprili hadi Juni na kufikia asilimia 0.61% ya Julai hadi Septemba 2023.
Pamoja na kufanya usimamizi katika kutekeleza shughuli za lishe katika wilaya watendaji wa kata wamekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwenye jamii inayowazunguka ili kusaidia jamii kujua na kutambua umuhimu wa Lishe kwa wananchi wa Lingido.
Pamoja na usimamizi na utekelezaji wa shuguli za lishe bado kumekuwa na mila na desturi potofu juu ya hali ya Lishe hasa katika jamii ya wafugaji ambazo zinawazuia wakina mama na watoto kula baadhi ya vyakula na hali hii inapelekea wakina mama wengi kukosa maziwa ya kutosha wanapokuwa kwenye uzazi, na hapa ndipo watoto wanapoanza kupungua uzito na kuingia kwenye utapiamlo.
Nae Ndugu Joshua Gadiye Afisa lishe shuleni Ameiomba jamii na wazazi wenye watoto mashuleni kuchangia upatikanaji wa chakula mashuleni ili watoto hao waweze kupata chakula wakati wanapokuwa shuleni kwani upatikanaji wa chakula hicho kitawasaidia watoto hao kutimiza ndoto zao, "Niombe ndugu wajumbe tusaidiane kuhimiza wazazi walio na watoto mashuleni wachangie chakula cha kutosha ili wawe na chakula cha akiba kitakacho tosheleza wakati wote isiwe leo kuna chakula na kesho hakipo",alisema ndugu Gadiel
Nae Afisa Kilimo Mifugo, na Uvuvi Ndugu Nestory Dagharo ameimbia kamati ya Lishe kuwa tayari Shirika la CONVOY OF HOPE limegawa jumla ya Tani 18 kwa kata za Mundarara na Matale B ikiwa na lengo la kuboresha lishe katika jamii
Vilevile Shirika la CONVOY OF HOPE limegawa kuku wasio pungua 1500 katika kata ya Mundarara ili kuboresha hali ya uchumi na hatimae lishe katika jamii.
Akisoma taarifa ya Lishe katika kitengo cha maendeleo ya jamii kwa kipindi cha Julai hadi Septemba ndugu Elmina Thadei Amesema ili kuboraha lishe kwa wanajamii Shirika la sauti moja limetoa msaada wa chakula kwa vikundi vitatu kutoka kata ya Longido Mairowa, na Olmolog wenye thamani ya Shilingi 5,187,000 ambayo imewasaidia sana kuokoa hali ya Lishe kwa kaya hizo.
Hali ya Lishe ya wilaya imekuwa ikiimarika siku hadi siku kwani tayari jamii inaendelea kuelimika na kufahamu umuhimu wa chakula bora kwa kufanya hivyo tutakuwa na kizazi chenye afya njema na chenye furaha.
"Ni jukumu la kila mmoja wetu aliopo hapa anakuwa mjumbe wa utekelezaji wa shughuli za lishe zinazofanyika katika jamii yetu ili kupata kizazi chenye nguvu kwa maendeleo ya Taifa letu michango na mazungumzo yetu yakawe sehemu ya utekelezaji sio maneno tu ili tutimize jambo la lishe katika jamii yetu. Alisema Daktari Mathew Majan Kaimu mkuu wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi alipokuwa akifunga kikao.
Vikao hivi ni endelevu vinavyotekelezwa katika kila robo ndani ya Halmshauri.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM