Kikao kazi cha wadau wa sekta ya Afya katika mkoa wa Arusha kimeendelea leo Mei 9, 2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Longido kikiongozwa na mwenyekiti ambaye ni Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. Wedson Sichalwe, huku hoja mbalimbali zikijadiliwa, mbinu tofauti kwa hatua muhimu za kuchukua lengo ni kuweka ulinzi, tahadhari dhidi ya kunusuru vifo vya uzazi na watoto.
Dk. Sichalwe amezungumzia swala la vifo vya akina mama, uzazi na watoto kuendelea kutokea ni kutokuwepo kwa ushiriki wa karibu baina ya jamii na wataalamu au waganga na wadau wa sekta hiyo, hivyo amedai kuwa kuna kila sababu ya kutafuta utatuzi wa nini chanzo cha vifo wapi pana mapungufu kwa kujadiliana na jamii, wataalamu pamoja na wadau kwa kutoa nafasi za mapendekezo, maoni na ushauri.
Vilevile amewasihi wadau wote wa Afya kutojitenga na jamii kwani kunauhitaji mkubwa wa kuwaelimisha wananchi ili wachukue hatua za haraka kuwahi hospitali pale linapotokea tatizo la kiafya kwa mama, jambo linalowasaidia wataalamu kunusuru maisha ya mama na mtoto kuliko kwenda wamechelewa jambo linalowapa ugumu wahudumu wa Afya.
Dk. Simon Chacha ambaye ni Mganga mkuu wa jiji Arusha amelitolea ufafanuzi swala la vifo hivyo kwa kusema kuwa hatua zimekuwa zinachukuliwa baada hatari na kwa wakati ambao huwezi nusuru maisha kwa asilimia mia .
Aidha amewataka wadau wa Afya kushirikisha taasisi zote za Afya zilizopo Mkoa wa Arusha na kuzipa vipaumbele ili kuwafikia wananchi wote na kutaka iundwe sheria inayowataka na kuwasisitiza akina mama kujifungulia hospitali .
Naye Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Arusha Denis Mgiye amewaomba wadau kutowaweka nyuma ofisi za Ustawi wa jamii kwani na wao wanayodhamana ya kufahamu kwa ukaribu matatizo yaliyo kwenye jamii.
Dk. Titus Mmasi DMO wa Monduli amebainisha changamoto zilizopo kuwa ni kushindwa kuwafikia na kuwahusisha katika vikao wananchi wote, kutowahusisha kamati ya ulinzi ya ustawi wa jamii ile hali wana mamlaka ya kutoa taarifa za maendeleo ya jamii pamoja jamii kutojitokeza kwa wingi katika mikutano.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM