Chama cha ushirika cha usafirishaji cha Kimana SACCOS kinachofanya biashara ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika barabara kuu ya arusha Namanga leo Tarehe 17.05.2018 wamemkabidhi mkuu wa wilaya ya Longido Mh. Daniel G. Chongolo mifugo 40 ya sementi yenye thanani ya Tshs. 600,000/=.
Lengo la chama ni kuunga juhudi na jitihada za serikali zinazofanywa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali wilayani Longido.
"Tumeamua kuunga mkono shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali ya Wilaya ya Longido, wamekuwa msaada mkubwa sana wakati tunaanza mpaka hapa tulipo fikia ambapo tunamiliki magari 6 sasa" amesema mwenyekiti Ndugu Rashid Massoud.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Daniel Chongolo amewashukuru sana Chama cha ushirika kwa kuamua kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuisaidia jamii, maendeleo ya wilaya yanajengwa na wananchi wenyewe tunashukuru sana kwa mchango wenu kwani unakwenda kubadilisha maisha ya wanafunzi, madarasa hayatoshi hivyo mchango huu tunaupeleka katika shule ya sekondari matale ilikwenda kuendeleza ujenzi wa upanuzi wa madarasa katika shule hiyo alisema mkuu wa wilaya ya longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM