Kamati ya fedha Utawala na Mipango imefanya ziara ya siku 2 kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu na Barabara inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Longido kwa siku mbili mfululizo tarehe31/08/na 01/09 /2023.
Utekelezaji wa miradi hii ya maendeleo katika Wilaya ya Longido inatekelezwa kwa Fedha zinazotolewa Serikali kuu, Kapu la Mama, BOOST, LANES II, TASAF, CDCF, SEQUIP pamoja na Mapato yake ya ndani zaidi ya Bilion 2.6 kwa ujumla wa fedha zote, ikiwa ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa Serikali katika kuleta Maendeleo kwa wananchi wake.
Kamati hiyo ya Fedha ya halmashauri ya Longido pamoja na wataalam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Simon Oltosoi imetembelea na kujionea miradi takribani 24 yenye gharama ya zaidi ya Bilioni 2,602,688,130.53 inayotekelezwa Wilayani Longido.
Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni Kituo cha Afya Gelai Lumbwa ambapo kamati imetembelea Ujenzi wa jengo la Mochwari, jengo la Upasuaji, Jengo la mama na mtoto, jengo la Wagonjwa wa nje pamoja na ujenzi wa jengo la maabara,
Miradi hii ya maendeleo kwa kiasi kikubwa ipo kwenye hatua za mwisho za ukamailifu wake ili iweze kutumika na kuwanufaisha wananchi waishio kwenye kata hiyo hata wa nje ya Halmashauri ya Longido, pia kamati imejionea na kujiridhisha ujenzi wa kituo cha Afya Ketumbeine sambamba na nyumba ya watumishi 3 kwa 1 inayojengwa kwenye kata ya Ketumbeine,Miradi mingine iliyotembelewa ni kama mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Mundarara, ujenzi wa madarasa Matatu shule ya Sekondari Tingatinga ,Jengo la Maktaba na Bweni katika sekondari ya Tingatinga, ujenzi wa shule Mpya ya sekondari Kamwanga,Ujenzi wa Shule ya Msingi Irkaswa, Ujenzi wa shule ya awali ya mfano Irkaswa, ujenzi wa nyumba ya watumishi Irkaswa , Ujenzi wa Matundu ya vyoo shule ya Msingi Lerang'wa sambamba na ujenzi wa madarasa matatu katika shule hiyo ya Lerang'wa pia kamati imetembelea na kuona ukamilishwaji wa majengo shule ya Sekondari Sinya, Kamati imejonea ujenz wa barabara ya jamii yenye urefu wa km za mraba 3.6,ujenzi wa Stand ya Malori Eworendeke na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi iliyopo Longido.
Pia kamati imetembelea miradi inayofanywa na vikundi mbali mbali vya kinamama vijana na watu wenye ulemavu vinavyonufaika na mikopo ya Halmashairi ikiwemo kikundi cha Juhudi kilichopo katika kijiji cha Longido na kikundi cha vijana Naibala Itubula katika kijiji cha Matale A, kikundi cha vijana Enyorata katika kujiji cha Irakaswa pamoja na kikundi cha wanawake kilichopo kijiji cha Gelai Lumbwa
Vile vile kamati ya Fedha Utawala na mipango imetoa ushauri mbali mbali kwa wenyeviti wa kamati za utekelezaji wa Miradi na viongozi wa kisiasa katika kila Miradi inayotekelezwa wilayani hapo kuwa waone namna njema ya kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora na kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ,Pia jamii ihamasishwe kuchangia miradi ya Maendeleo.
"Waheshimiwa madiwani pamoja na wataalam sote kwa pamoja tunapaswa tuweke jitihada kubwa sana katika kuisaidia serikali juu ya Miradi tuliyopewa tunayo dhamana kubwa sana ya kuhakikisha tunaisimamia kwa weredi mkubwa sana mana miradi ni yetu sote sisi Wananchi wa Longido na Serikali kwa kutujali na kutupenda sisi wananchi wa Longido imetupatia pesa nyingi sana kwenye kutekeleza Miradi hii basi tumsaidie mama Samia kwenye kusimamia utendaji wa kazi hizi kwemye Halmasahauri yetu kila mmoja wetu aone analo jukumu katika kusimamia utekelezwaji wa Miradi hii kwa manufaa wananchi wa Longido ili wapate huduma bora kwenye nyanja zote za Elimu Afya Maji na Hata barabara. "Alisema Mheshimiwa Simon Oitesoi.
Miradi yote ya Maendeleo iliyotembelewa na kamati hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.
*Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM