Shirika la LIONS CLUB of ARUSHA katika hatua ya kuendelea kusaidia watu waishio vijijini limetoa msaada wa huduma ya macho katika Hospitali ya Wilaya ya Longido pamoja na kukabidhi miche ya Miti 70 kwa Afisa misitu wa Wilaya hiyo ili kuboresha utunzaji wa mazingira, Mei 19, 2019.
Akizungumzia zoezi la utoaji wa msaada huo Mkurugenzi wa Lions Club of Arusha Balwinder Singh Bansal amesema kuwa shirika linalenga kusaidia maeneo yote ya Vijijini katika mkoa wa Arusha yenye uhitaji katika Elimu, Afya, Mazingira na Ustawi wa jamii.
Vilevile Bansal amesema kuwa huduma ya macho itasaidia kuendelea kwa shughuli za hapa na pale kwa kiasi kukubwa hasa kwa wanachi ambao walikuwa hawaoni karibu na mbali “wananchi wataanza kuona vyema sasa maandishi, kuchambua vyakula n.k. na wale wasiokuwa na uwezo wa kununua miwani wamepatakulingana na matatizo walionayo baada ya vipimo kutoka kwa wataalamu” amesema Bansal
Ameendelea kusema kuwa Lions Club of Arusha inatambua uwepo wa watu kama hawa na itaendelea kuwasaidia kwa kadri iwezekanavyo na kutoa ushauri wa kitaalamu wa kufika Hospitali watakazoelekezwa mara kwa mara kwa matibabu zaidi wale wenye matatizo kama Mtoto wa jicho n.k., pia katika mazingira amefafanua kuwa Longido inakuwa na ukame kwahiyo watashirikiana kuumaliza.
Naye Mratibu wa Lions Club of Arusha Maswanya Yusuf ameelezea jinsi walivyotambua uwepo wa wananchi wenye nia ya kulitumikia taifa lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu ni baada ya kuona waliowengi wanapatikana Vijijini. Ambapo katika zoezi hilo wamejitokeza wananchi wengi swala ambalo limepelekea zoezi kuanza asubuhi majia ya saa 03:00 mpaka 12: jioni.
Kwa upande wake Mratibu wa Macho Wilaya ya Longido Gustaph Thadeus Materu amesema lengo la huduma hii iliyotolewa na Lions Club of Arusha ni kupima macho na kutoa huduma kwa watakaogundulika na matatizo, na kwa wale watakaogundulika wana ugonjwa kama mtoto wa jicho watapata huduma katika hospitali ya St. Elizabeth vilevile watakaoshindikana watagharamikiwa gharama za matibabu katika Hospitali ya KCMC.
Materu amebainisha chanzo cha magonjwa kama ya macho kuwa ni Uzee, Vumbi, maji machafu, kisukari n.k. Pia ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kufika hospitalini hapo na kuonana na wataalamu kwa matibabu zaidi.
Akipokea miche ya miti 70 Afisa Misitu wa Wilaya ya Longido Boaz Mtokoma amewapongeza Lions Club of Arusha kwa msaada huo huku akiahidi kupanda miti hiyo kwa wakati katika maeneo mbalimbali “Kwa niaba ya mkurugenzi wa Wilaya nitoa shukrua za dhati kwenu na muendelee kutukumbuka tunaomba zaidi na zaidi bado tuna uhitaji mkubwa wa miche ndani ya Wilaya yetu” alisema Boaz
Boaz Mtokoma ameendelea kusema kuwa shukrani za dhati ziwafikie watu pamoja na mashirika binafsi na serikali kwa misaada ya miche ya miti inayoendelea kutoa wilayani Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM