WIZARA Ya maji na umwagiliaji inatarajia kutoa shilingi million mia moja na saba(100.7 million ) kwa ajili ya ujenzi Wa miundombinu ya Mifugo kunywa maji( cattle turf)wilayani Longido Mkoa Wa Arusha,kwa lengo la kuondoa migogoro baina ya wafugaji na serikali juu ya uharibifu Wa miundombinu ya mradi Wa maji kutoka mto simba Wilaya ya siha Mkoa Wa Kilimanjaro uliogharimu zaidi ya sh16 billion fedha kutoka serikali kuu.
Akielezea katika ghafla ya makabidhiano ya mradi huo kutoka katika mamlaka ya maji Wilaya ya Longido na kusimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi Wa mazingira Mkoa Wa Arusha (AUWSA) Prof Kitila Mkumbo ambaye ni katibu mkuu wizara hiyo alidai kuwa ni uamuzi Wa serikali ikiwa ni sehemu ya agizo la Rais Magufuli kuwa mamlaka zote za maji zijitegemee.
" Serikali imeamua kutenga sekta Hii ya maji kujitegemea ili ziweze kufanya kazi kwa kasi na kuhakikisha serikali za mitaa zinapata maji ikiwa na usimamizi mzuri ,akitolea mfano kama Tanesco ilivyo na wakala wa umeme vijijini Rea pamoja na Tan Road ilivyo na wakala ambao ni Tarura" alifafanua
Prof Kitila alisema Lengo hasa ni kuanzishwa kwa wakala Wa maji safi na usafi Wa mazingira vijijini,ikiwa ni kupanga na kusimamia uwezeshwaji Wa maji vijijini na sasa serikali ipo katika hatua ya kusimika mamlaka hiyo rasmi,hivyo mamlaka ya maji Longido kuanzia sasa itakua chini ya usimamizi Wa mamlaka ya maji Mkoa Wa Arusha (AUWSA)
Aidha alidai kuwa changamoto kubwa katika sekta ya maji ni baadhi ya miradi ya miaka ya nyuma kutokukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya wakandarasi kushindwa kutekeleza majukumu yao ,akitolea mfano mradi wa maji mkoa wa kilimanjaro ulioanza tangu mwaka 2014 lakini hadi sasa hauja kamilika
"Nawapongeza viongozi wote Mkoa Wa Arusha na hata ngazi ya Wilaya ya Longido,mradi Huu mmeusimamia vizuri ,lakini naomba hadi itakapo fika mwisho Wa mwezi Huu wale wote waliokua wamejiandikisha katika mpango Wa kupata maji waunganishiwe na kwa sasa wauziwe ndoo ya maji sh 20 wakati Mamlaka AUWSA ikiendelea na mikakati ya kupanga bei kwa kushirikiana na Ewura" aliomba Prof Kitila
Hivyo Prof Kitila ametangaza rasmi Leo mradi mkubwa Wa maji kutoka chanzo cha maji mto simba wilaya ya siha mkoani kilimanjaro uliotekelezwa na serikali kuu katika wilaya ya Longido wenye thamani zaidi ya Shillingi Billion 16 ikiwa ni fedha za ndani umekamilika na utakua chini ya usimamaizi Wa mamlaka ya maji safi na usafi Wa mazingira Mkoa Wa Arusha (AUWSA)
Hata hivyo mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo aliagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa watu 21 waliohusika kuhujumu mradi huo kwa kutoboa bomba za maji,kwani serikali imetoa fedha nyingi sana haiwezekani kuwavumilia wachache wanao haribu mradi huo
" Naagiza Mkuu Wa Wilaya kamata wale wote walio husika kutoboa mabomba na wafikishe mahakamani,Lakini pia niwaombe wananchi Wa Longido tunzeni mradi huu " Mhe. Gambo
Awali Mkuu Wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema changamoto iliyopo kupitia mradi huo ni wananchi (wafugaji) kutoboa mabomba ili Mifugo yao ipate maji,na hali hii inasababishwa na ukame uliopo wilayani hapa,hivyo alisisitiza serikali kukamilisha ujenzi Wa mbauti ( cattle turf) ili Mifugo ipate maji kwa wakati.
Mkurugenzi Wa maji safi na usafi Wa mazingira Mkoa Wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruthi Koya alisema Wilaya ya Longido ilikua na upungufu Wa maji safi na salama,lakini kupitia mradi huu maji safi na salama yapo na yanatarajiwa kuhudumia watu elfu 26,142 ifikapo mwaka 2024
" Mji wa longido unawakazi elfu 16,712 kwa sasa hivyo bado kuna maji mengi ya ziada ,na lengo hasa la serikali nikuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama " Mhandisi Koya
Makabidhiano hayo yamehudhuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Mhe. Sambore Molloimet, Mkurugenzi mtendaji wa Wailaya hiyo Ndug. Jumaa Mhina pamoja na wakuu wa Idara zote zinazohusika na Mifugo na Uvuvi, Maji afi na Maji taka n.k.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM