Katika harakati za kuimarisha ulinzi na usalama shule ya sekondari Longido iliyoko wilayani longido mkoani Arusha imepokea mifuko 200 ya simenti kutoka kampuni ya mission kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule jana tarehe 14, disemba 2017.
Wakati akitoa shukrani zake za dhati mkuu wa shule ndg.Danieli g.Ntemi ameweza kueleza kuwa wazo hilo lilianza kipindi shule yao kuungua moto hivyo kuanza shughuli ya ujenzi rasmi mnamo januari 2017 kwa nguvu za wazazi lakini kwa kusuasua kwani ilikuwa ni kama ndoto ambayo wasingeweza kutekeleza.
Ndg.Daniel g.Ntemi ameendelea kufafanua kuwa wazo lao lilipata nguvu rasmi wakati wa mahafali ya kidato cha sita tarehe 8,April2017 baada ya kuahidiwa na mgeni rasmi katika hiyo mahafali mkurungenzi wa kampuni ya mission Bw.Michael Manthakis kwa kuwa ahidi tani 30 za simenti kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Pia ahadi hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 12/07/2017 ambapo tani 10 za simenti kati ya tani 30 zilitolewa kwani kwa kufanya hivyo si kwamba ilishindikana kutolewa tani zote 30 kwa wakati moja bali nikwa angalizo aliyoito bw.michael ya kuwa simenti zinaweza kuisha muda wake hivyo kuletwa kwa awamu tatu ambapo awamu mbili kukamilishwa kwa sasa nakusalia awamu moja tu katika ahadi hiyo.
Vile vile mkuu wa shule ndg.Ntemi ameweza kuwa fafanulia hatu waliyoifikia katika ujenzi huo kuwa upande wa kusini 440m na 35cm,upande wa mashariki 205cm na kwa upande wa magharibi 99m na 60cm hivyo kusema ujenzi bado unaendelea vizuri kwa hatua hiyo ya msingi.
Hata hivyo katibu tarafa ndg.Mtasigwa naye ameweza kutoa shukrani zake kwa kampuni hiyo akieleza moja ya changamoto kubwa ambayo inaikumba shule hiyo ni kutokuwa na uzio swala ambalo linahatarisha usalama wa shule kwani mtu yeyote anaweza kuingia kupitia popote na kufanya anavyojiskia kufanya ,huku akiwaasa wanafunzi kuwa kwakufanya hivyo si tu shule ipendeze ni pamoja na matunda mazuri yaonekane kutoka kwenu kwani kupendeza kwa shule ni pamoja na matokeo mazuri.
Aidha Afisa elimu sekondari ndg.Gerison Mtera ameipongeza kampuni hiyo kuonesha moyo wa mkubwa kwa kushirikiana na jamii hiyo kufanikisha suala hilo huku akiwataka uongozi wa shule usimamie vizuri zoezi hilo la ujenzi kwani msaada unapotolewa bila kuufanyia kazi ni bure pia ni kumkatisha tamaa aliyejitoa kufanikisha kazi hiyo nakuwa sisitiza pia kuwa fuatilia waliowaahidi bila kutekeleza ahadi zao kwa kukamilisha mapungufu ya shule hiyo .
Hivyo basi uongozi wote wa shule ,wanafunzi,na viongozi kutoka ngazi ya halmashauri ya wilaya Longido wametoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya mission ya bw .michael Manthakis kwa kutekeleza ahadi yake kwa muda bila kusukumwa wala kulazimixhwa kwani amekuwa mfano kati ya wadau wote waliowahi kutoa ahadi kwa kuitekeleza ipasavyo.
Vile vile wamemtaka mwakilishi wa meneja huyo ndg.Damasi Rumangisa kumshika mkono meneja atakaporejea kuwa ni ishara ya shukrani zote zilizotolewa na Taasisi,bodi ya shule pamoja na wazazi huku wakimsisitza kuwa bado shule yao inauhitaji mkubwa hivyo wasisite kutoa msaada wao watakapohitaji.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM