Mkuu wa wilaya ya Longido Mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi leo tarehe 10/07/2023, amepokea mradi wa chakula toka Shirika la World Vision kwa ajili ya shule za msingi 30 zilizopo katika kata ya Ketumbeine ambazo zina zaidi ya wanafunzi 11,726.
Akikabidhi chakula hicho, Mratibu wa world Vision kata ya Ketumbeine Ndugu Peruth Daudi kwa shule hizo 30 za msingi, World Vision imetoa jumla ya gunia 1140 za Mahindi, Gunia 281 za Maharagwe pamoja na Ndoo 274 za Mafuta ya kupikia zenye ujazo wa lita 20 ambavyo vimegharimu takribani Shilingi Milion 175 za kitanzania.
Mheshimiwa mkuu wa wilaya amelishukuru shirika la world Vision kwa kuona sababu ya kutoa msaada huo wa chakula kwa watoto wa shule za Msingi katika Wilaya yake "Nimepita nimeona chakula mashuleni, kama tunavyojua uwepo wa chakula mashuleni kunaongeza chachu ya wanafunzi katika kujifunza".Alisema mheshimiwa Ng'umbi.
Serikali inatambua mchango wa wadau na mashirika mbalimbali kwenye elimu, hivyo basi inaunga mkono jitihada za Shirika la World Vision kwenye kusaidia wanafunzi haswa wa shule za msingi.
Mheshimiwa mkuu wa wilaya amelipongeza shirika la World Vision kwa kutimiza Afua za lishe kwa wanafunzi "Kwa kuwa watoto wanakula shuleni wote tumeona wamependeza na wana afya njema" aliongeza Mkuu wa wilaya.
Naye Ndugu Grace Mghase kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido amewaasa shule zilizonufaika na chakula hicho kukitumia kwa manufaa ya walengwa na si vinginevyo. Kwa kufanya hivyo kunarahisisha matumizi ya bajeti ya chakula kwa muda mrefu, na amewaasa wazazi kutojibweteka katika uchangiaji wa chakula mashuleni.
Shirika la World vision limekuwa likifanya vizuri kwenye maendeleo haswa ya chakula mashuleni kwenye wilaya ya longido haswa kata ya Ketumbeine.
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM