Halmashauri ya Wilaya ya Longido chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndug. Jumaa Mhina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini Tanzania imetoa Elimu kwa waandishi wasaidizi wa uchaguzi ili kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura.
Mafunzo hayo yametolewa na Maafisa Uandikishaji ngazi ya jimbo na Maafisa Tehama wa Wilaya katika ukumbi wa Halmashauri Longido leo julai 11, 2019, mafunzo ambayo yameudhuriwa na Maafisa waandikishaji wasaidizi na BVR operator wa kata 18 zote za Wilaya ya Longido.
Awali kabla ya Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji Ndug. Mhina ambaye alikuwa mwenyekiti katika mafunzo hayo pia amesimamia zoezi la ujazaji wa Fumu za kiapo ambapo amewataka waandikishaji wasaidizi kuhakikisha hawana chama chochote.
Ndug. Mhina amefafanua kuwa usimamizi hauhitaji kada yeyote wa chama badala yake ni watumishi wa tume pekee . Mkurugenzi amewataka kujitoa kwenye chama kwanza, kujaza majina yao matatu , maeneo wanakotokea vilevile kuweka kiapo kuwa hawatakuwa na kipendeleo wala upande wowote na mwisho kuweka sahihi ya kiapo hicho.
Miongoni mwa washiriki wa utoaji mafunzo hayo ni Saul Nleya ambaye ni Mratibu wa uandikishaji wa Mkoa, ambaye amewataka waandikishaji hao kuwa zipo sehemu katika Mkoa wa Arusha ambazo ni Wilaya za Longido,Ngorongoro na nyinginezo ambazo zipo katika mipaka ya nchi zinauhitaji mkubwa wa umakini katika kuandikisha ili kuhakikisha wanawaandikisha walio raia wa Tanzania na watambuliwe kutoka kwa viongozi wa ngazi ya vitongoji, vijiji, kata mpaka wilaya.
Aidha Mhe. Jaji (R) Mbarouk Salim Mbarouk ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi ameagizi kufuata sheria, taratibu, kanuni, na maelekezo watakayopewa waandishi hao bila kusahau taratibu za tume ya taifa ya uchaguzi.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Zanzibar Thabit Idarous Faina amewataka kuwa na umakini, weredi pamoja na uwajibikaji muda wote wa uandikishaji kama kufika kituo muda mwafaka (08:00) asubuhi mpaka (12:00) jioni.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM