Waziri wa Afya, Vijana, Ajira, Wazee na Watu wenye Walemavu Dr. Ummy Mwalimu amesema Magonjwa ya mripuko yasitegemee Serikali tu ichukue hatua bali ni kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anachukua hatua za haraka pindi anapoona dalili zake pamoja na kujikinga juu ya janga hili.
Ameyasema hayo mapema leo juni 11, 2019 wakati akifungua rasim Zoezi la siku nne la kuigiza hali halisi ya kukabiliana na vitisho vya magonjwa ya maambukizi maarufu kama “ZOEZI LA KUINGIZA NYANJANI KWENYE MPAKA WA NAMANGA TANZANIA NA KENYA” ufunguzi huo umefanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya Namangan a kuhudhuliwa na Viongozi mbalimbali kutoka Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda na wawakilishi kutoka nchi wanachama wa zoezi hilo.
Dr. Ummy amesema kuwa serikali ya Tanzania magonjwa kama Homa ya bonde la ufa inalichukulia swla kubwa hivyo inaendelea kuzuia na kujikinga kwa kuweka utayali wa kupambana kupitia Sekta zote husika za Afya, Kilimo, Ufugaji,ulinzi,Utalii pamoja, biashara na kijamii ili kuweka usalama wa Binadamu na Wanyama pamoja na Kupunguza kupoteza rasilimali nguvu watu swala linalorudisha nchi nyuma katika ujenzi wa maendeleo.
Aidha Dr. Ummy ameeleza kuwa zoezi hilo litaongeza utayari wa kuangalia sehemu za maboresho kwa mapungufu yatakayojitokeza na kuwasaidia Wananchi kuweka utayali wa kubadilishana taarifa huku wakichukulia swala hilo kuwa ni miongoni mwa kazi kama isemavyo kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU!.
Awali akizungumza kwa niaba ya waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa wizara kwa kushirikiana na Serikali imejipanga kuhakikisha inaunga mkono zoezi hilo lenye lengo la kujikinga na magonjwa ya Bonde la ufa ambayo yanatabia ya kujirudi ili kuondoa vikwazo katika ujenzi wa uchumi na Kupunguza ulemavu kwa Binadamu na wanyama.
Kwa upande wake mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dr. Tigest Ketsela Mangestu amesema kuwa 75% ya magonjwa ya mripuko yanatokana na Nyama anazokula binadamu na kwa mwaka 2007 vifo 1500 kutoka Tanzania na Kenya vilitokea, huku akifafanua kuwa vifo vingine utokea kwa nchi kushindwa kuzuia waamiaji haramu licha ya kwamba swala hilo lipo kisheria na viongozi wapo wanaotakiwa kusimamia.
Naye Gavana wa Kajado nchini Kenya Martine Mshisho ametoa wito kwa jamii kuwa swala la kubadilishana taarifa kwa wakati na haraka ni muhimu kwa magonjwa ya bonde la ufa hayahitaji viza wala kadi za kusafiria hivyo tusikubali kuyakaribisha kwenye jamii zetu. Gavana Mshisho amewaakikishia usalama viongozi na wadau waliohudhulia zoezi hilo kuwa wapo salama na wajisikie huru.
Zoezi hilo limehudhuliwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Frank Mwaisumbe ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewaakikishia uslama kwa kipindi chote cha mafunzo popote watakapokwenda huku akiwakaribisha kuja Arusha kujionea vivutio vya Utalii baada ya zoezi kumalizika, vilevila Mkurugenzi Mtendaji amejumuika na wataalamu kuhakikisha zoezi linaenda safi.
Zoezi la “ZOEZI LA KUINGIZA NYANJANI KWENYE MPAKA WA NAMANGA TANZANIA NA KENYA” lemeendelea katika maeneo mbalimbali Nchini Tanzania na upande wa Kenya, Kwa Tanzania wataalamu hao wametembela katika vituo mbalimbali ambavyo vimeonekana magonjwa ya bonde la ufa utokea ikiwemo kituo vya huduma za Afya Namanga, ketembelea wakuu wa Idara husika Halmashauri kuu Longido vilevile Maeneo ya Machinjioni ya nyama Namanga.
Dr.Peter Mkama ambaye ni Mtaalamu Mwendeshaji wa Maabara Tanzania ametoa ufafanuzi wa namna ya kutambua vimelea vya magonjwa ya mripuko, jinsi ya kutambua aina zake, namna ya kuviondoa kwa mgonjwa na kuviangamiza, ufafanuzi huo ameutoa wakatia akiwa katika Maabara ya kisasa ya EAC MOBILE LABORATORY UNIT shule ya msingi Namanga.
Dr.Mkama amesema zipo sehemu kuu tano ambazo upitia mpaka kutambua majibu ya vimelea vya ugonjwa. Moja amesema ni mapokezi na kutambbua sampuli ili kuweza kufungua, Mbili kufungua sampuli na kutakasa kwa kuua virusi vya maambukizi, tatu kuvina vina saba vya sampuli au vimelea waliopo kwenye virusi, nne kuweka na kuandaa vitenganishi vinavyochanganywa na vina saba vya kwanza ili kwenda kwenye ugunduzi, tano na mwisho kufanya ugunduzi kwenya Machine ya PCR. Majibu upelekwa kwa Daktari aliyeomba kipimo.
Naye Edwrd William ambaye ni Mkurugenzi katika machinjio ya nyama Namanga amesema wanyama wanaochinjwa kutoka Tanzania na Kenya na vigumu kumtambua mnyama mwenye ugonjwa hasa ng’ombe akiwa mkubwa kiumri hivyo upima nyama baada ya shughuli ya kuchinjwa kumalizika.
Adha amesema wanapotambua mnyama huyo anavirusi basi waliohusika kuchinja wote,nyama yenyewe wanahimizwa kutotoka nje ya eneo la machinjio huku wakifanya mawasiliano na wataalamu watoa huduma za Afya za Wanyama na Binadamu ikiwa pamoja na kuwasiliana na mnyama alikotokea ili wachukue hatua za haraka.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM