Walengwa 43 wa kaya maskini katika kijiji cha Orbomba leo tarehe 20/04/2023 wamepewa mbuzi takribani 164 aina ya ISIOLO na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF),makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya kijiji cha Orbomba.
Akikabidhi mradi huo wa mbuzi aina hiyo ya ISIOLO kwa walengwa 43, Mheshimiwa Marko Ng'umbi mkuu wa Wilaya ya Longido amewataka wanakaya kuwatunza mbuzi hao kwa lengo la kuondoa umaskini kwenye kaya. Mbuzi hao wakiwatunzwa vizuri watawasaidia kuongeza kipato kwani tunafahamu kuna faida nyingi sana kwenye mifugo hii ya mbuzi ikiwepo nyama, Maziwa, na wanapozaliana tutapata mbuzi wengi hapo sasa ndipo mnaweza kuwauza nakujipatia pesa kwa ajili ya chakula, mavazi, makazi bora pamoja na kusaidia kuwapeleka watoto shuleni.
Pamoja na hayo Mheshimiwa mkuu wa wilaya amewaasa wanakaya kutowapeleka sokoni mifugo hiyo hivi karibuni badala yake wawatuze mpaka watakapozaliana ndipo wanaweza kuwapeleka sokoni mana watakuwa wengi,kwa kuwa mradi umelenga kuongeza kipato kwa kaya hizo maskini. sambamba na hilo amewaomba wahakikishe mifugo hiyo inakuwa salama, "Ndugu zangu sitopenda kusikia mbuzi hawa tuliowagawia leo wanakufa au wamepotea ama wamepata madhara yeyote yale badala yake nitafurahi nikisikia wako vizuri wana afya njema na wameongezeka kwa maana wamezaliana ili tujikwamie kiuchumi, badala ya kula mlo mmoja ama kushinda njaa na kulala njaa kabisa sasa tukiweza kuwatunza tutakula milo mitatu bila shida wala tatizo lolote "Alisema Mheshimiwa Ng'umbi
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Longido ndugu Stephen Ulaya ameishukuru Serikali kwa kuwezesha kufanikisha mradi huo kwa kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF awamu ya III,vilevile amewasihi sana wanakaya kuwatunza mbuzi hao ili waweze kuwasaidia kiuchumi
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji na wanakaya hao wa kaya maskini mwenyekiti wa kijiji cha Orbomba ndugu Lashilo Alais Ameishukuru wadau wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF pamoja na serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wake na kuwapatia mbuzi hao kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na ameahidi kuwatunza kwa kila hali ili waweze kuwaletea manufaa katika kuongeza uchumi wa kaya.
Pia ameongeza kwa kuiomba Serikali kuwakumbuka zaidi kwani bado kuna kaya nyingi zinahitaji msaada kama huu ili ziweze kujikwamua na wimbi hili la umaskini. "Tunaiomba Serikali iendelee kutufikiria kwani bado kuna wananchi wengu huku kwetu wanauhitaji, hawa ni wachache tu ila bado wako wengi kijijini maisha yao ni changamoto "Alisema ndugu Kashilo Alais.
*JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM