Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa timu za utekelezaji wa mradi wa Boost ngazi ya Mkoa na Halmashauri yamezunduliwa rasmi mkoani Arusha na Mheshimiwa Angella Kairuki tarehe 13/12/2022 ikijumisha kanda ya kaskazini mikoa ya Arusha, Manyara na Singida
Akizindua mafunzo hayo ya siku mbili kwa wajumbe takribani 274 wanaounda team ya kufanikisha mradi wa Boost katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ilboru iliyoko mkoani Arusha mh waziri Angela Kairuki amewaaomba wajumbe kusimamia mradi huo ambao umelenga katika kuborosha elimu katika ngazi ya shule za msingi kwa madarasa ya awali na darasa la kwanza , ikiwa ni samabamba na kuboresha mazingira ya nje na ndani ya kujifunza na kufundishia ikiwemo madarasa pia kuongeza ujuzi wa watoto ili waweze kuwa na uwezo wa kuhesabu, kusoma na kuandika,kuongeza mzunguko kwa wanaomaliza elimu ya msingi ili kuweza kutimiza malengo yao na kuongeza umahili wa TEHAMA kuanzia ngazi ya awali mpaka chuo kikuu.
Mradi huu wa Boost ni mpya na utatekelezwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania mh waziri amewataka wajumbe kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa na Ofisi ya Rais Tamisemi pia amewaasa waratibu wa mradi katika kutekeleza mradi huu kufuata taratibu za manunuzi bila kubadilisha pale panapobidi kubadikisha basi kutoa taarifa ama ushauri kwenye ofisi husika yaani OR - TAMISEMI.
Kutokana na tathmini iliyofanyika Serikali imepata udhamini wa kiasi cha Tsh Tirion 1.15 kwa ajili ya kukamilisha Afua nane zilizowekwa. Ili kuweza kukamilisha mradi huu wa Boost tunapaswa kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye hafua zote nani kwani mradi huu ni "LIPA KWA MATOKEO"
Nimefurahishwa na uundaji wa Team hizi katika Mikoa ili ikiwa ni kuwa na lengo la kufanikisha shughuli zote za elimu ivyo niwaombe wajumbe kukamilisha Afua zote zikiwemo pamoja na kujenga madarasa 12000 nchi nzima, utekelezaji wa shule salama 1000, kuongeza idadi ya uandikishaji kwa madarasa ya awali na darasa la kwanza, utekelezaji wa Elimu wa walimu kazini ili kuwajengea uwezo katika ufundishaji, utekelezaji wa TEHAMA, kuboresha zana za ufundishaji, sambamba na kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi.
Aidha Waziri Angela ameitaka team kuwa makini wakati wa kujifunza ili kujua vema mradi na hatimae kuutekeleza vema kwa maslahi ya nchi kwa ujumla "ufanisi wa mradi huu uko mikononi mwetu"Alisema Mh Angela Kairuki
Ili kuweza kufanikisha mradi huu team ya kusimamia mradi imeishauriwa kufuata masharti ya mradi ikiwa ni kuzingatia sheria, kanuni na mwongozo wa mradi,utunzaji wa nyaraka zote muhimu kwa usahihi, mipango itayopangwa ifuatwe bila kuchepushwa kwa namna nyingine, kuimirisha uhusiano mzuri na jamii, kuepuka mianya yote ya rushwa katika utekelezaji wa mradi, kufanikisha mradi kwa muda uliowekwa.
Niwaombe ndugu zangu tuwe mfano mzuri katika kutekeleza mradi na sio kukwamisha maana sheria itachukuliwa kwa yeyote atakaebainika kuwa chanzo cha kukwamisha mradi hii ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Aidha waziri amemshukuru Dr Samia Suluhu Hasaan kwa kuona ipo haja ya kuborosha shule zetu za msingj hususani kwa madarasa ya awali na darasa la kwanza.
*KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM