• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO AWATAKA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUTUNZA VIFAA NA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

Posted on: December 5th, 2024

Shemzigwa: "Tunzeni Vifaa, Fanyeni Kazi kwa Uadilifu"!.


Wilaya ya Longido imehitimisha siku ya pili ya mafunzo ya uandikishaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata. Mafunzo haya yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa lengo la kuwawezesha wasimamizi hao kutekeleza majukumu yao kwa umakini na weledi.


Akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Nassoro Shemzigwa, alitoa wito kwa washiriki kutunza vifaa watakavyokabidhiwa na Tume, akisisitiza kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa kufanikisha zoezi hilo. "Tutunze vifaa hivi kama mali ya taifa, na zaidi, tufanye kazi kwa kufuata sheria na taratibu tulizoelekezwa. Lengo letu ni kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa anapata nafasi ya kujiandikisha," alisema Shemzigwa.


Aidha, Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Bw. Terevaeli Mbise aliipongeza Tume Huru ya Uchaguzi kwa juhudi zake za kuhakikisha mafunzo haya yanafanyika kwa kiwango cha juu. “Mafunzo haya ni muhimu sana kwa wasimamizi wa ngazi ya kata. Tumejifunza mengi na tunaahidi kuyatekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuhakikisha kila mkazi wa kata husika anashiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu,” alisema.


Kwa upande wake, Afisa mwandikishaji  ngazi ya jimbo Bw Nevilling Lymo aliwashukuru washiriki kwa bidii waliyoonyesha katika mafunzo hayo. Alisema kuwa juhudi walizoweka ni ishara ya dhamira yao ya kuhakikisha zoezi linafanikiwa. "Napenda kuwapongeza kwa kujifunza kwa moyo wote. Maarifa haya ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uboreshaji wa daftari unafanyika kwa usahihi na uwazi," aliongeza.


Washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuridhishwa na mafunzo waliyopokea, wakisema kuwa yamewaongezea maarifa muhimu ya kutekeleza majukumu yao kwa umakini mkubwa.


Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, hatua muhimu kuelekea chaguzi zijazo. Hii ni juhudi ya kuhakikisha kuwa demokrasia ya nchi inaimarika kwa kuwapa wananchi fursa ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya kitaifa.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WA UMMA April 12, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA May 15, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA June 25, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • KAMATI ZA MTAKUWWA ZAIMARISHWA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA NAMANGA

    August 22, 2025
  • View All

Video

MKUU WA WILAYA YA LONGIDO AUNGANA NA RC KIHONGOSI KWENYE JOGGING YA TANZANIA SAMIA CONNECT
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.