Leo tarehe 11-11-2019 wajumbe wa Baraza la madiwani wa halmashauri ya Longido wamefanya mkutano wa kawaida katika ukumbi wa JK Nyerere ulioko Halmashauri ya wilaya ya Longido. Mkutano huo ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bwana Gerson Mtera na Mh Simon Oitesoi Diwani kata ya Gelai Lubwa ulikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kupitia maazimio yote ya mkutano uliopita na utoaji wa taarifa wa utekelezaji wa kata kwa kipindi cha Julai mpaka septemba 2019.
Madiwani hao waliweza kuwasilisha taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji, utekelezaji wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi na afya.
Katika uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji waheshimiwa wajumbe madiwani wa kata walitoa taarifa mbalimbali kutoka katika kata zao ikiwemo utekelezaji wa miradi mipya na inayoendelea, mafanikio , changamoto na njia za jinsi ya kutatua changamoto hizo.
baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni pamoja na utoro wa wanafunzi mashuleni, upungufu wa vyumba vya madarasa ,nyumba za watumishi yaani waalimu, uhaba wa malisho ya mifugo, usafiri , maji safi na salama katika maeneo yao,madawati na vitendea kazi kwenye ofisi za umma.
Pia baraza la madiwani walimtaka afisa kilimo wilaya Ndugu Edward Kasiga kutoa vibali vya kupewa mahindi katika kata uzingatie uhitaji na sio kiwango kimoja kwa kata zote kwani kuna baadi ya kata hazina uhitaji na mwisho walikubaliana kuwa ugawaji wa mahindi ili kukabiliana na mfumuko wa bei katika kata mbalimbali ufanyike kwa kutegemea uhitaji wa kata husika kwani kuna baadhi ya kata hazina uhitaji kabisa ya mahindi hayo.
Mkuu wa wilaya ya Longido Ndugu Frank James Mwaisumbe alipata nafasi ya kuongea kwa kifupi na alisisitiza baadhi ya mambo muhimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa, uanzishaji wa shule ya kidato cha tano na sita katika shule ya Endument kwa ajili ya kuhamisisha wanafunzi kupata nafasi ya kuchukua masomo ya sayansi. Pia mkuu wa wilaya alisisitiza ugawaji wa mahindi kwa bei nafuu ili kuepukana mfumuko wa bei kwa kuzingati uhitaji.
Mh Simon Oitesoi alifunga kikao saa 7.00 mchana kwa kupata chakula cha pamoja na wajumbe wote.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM