Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Mrisho Mashaka Gambo ahitimisha ziara yake ya siku tatu wilayani Longido.
Mh Gambo amehitimisha ziara hiyo tarehe 16/5/2018 ambayo ilianza tarehe 14/5/2018 kwa kupitia hoja za CAG pamoja na wataalam wa Halmashauri ya Longido, lakini pia alipata muda wa kuongea na wananchi wa kata ya mundarara na kusikiliza changamoto zote ikiwa ni pamoja na changamoto ya miundombinu na kuaidi kuitatua kupitia TARURA lakini pia changamoto ya mawasiliano kwani hakuna mtandao wa simu unaopatikana katika kata ya mundarara na kuahidi kulifanyia kazi ndani ya muda mfupi
Aidha Mhe Gambo alikagua vituo vya afya vinavyojengwa vya Eworendeke na Engarenaibor na kupongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo unaojengwa kwa kutumia mafundi (force account) na kusimamiwa na Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri.
Kadhalika Mh.Gambo aliweka jiwe la msingi katika Maabara ya shule ya sekondari ya Ketumbeine na kuongea na walimu wa shule hiyo ambapo akiweza kuelezewa changamoto zinazowakabili na kutoa ahadi ya kuzifanyia kazi
Mh. Gambo alihitimisha ziara yake kwa kukagua chanzo cha Maji cha mto Simba wilayani siha kinacholeta maji Longido.
Katika ziara yake Mh.Gambo aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Daniel Chongolo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mwl.Gerson Mtera, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Esupat Ngulupa ,Wataalam kutoka Sekretariet ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Ndg Richard Kwitega. Pia walikuwepo wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Longido na Waandishi wa habari.
Mh.Gambo aliwashukiru Watumishi na kuwaasa wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali yao chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ina nia njema na ya dhati kwa watumishi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM