wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wa Mkoa leo tarehe 7/08/2023 ameanza ziara yake kutembelea na kujionea miradi mbalimbali ya maendelaeo iinayotekelezwa Wilayani humo.
Akizungumza na na viongozi wa wilaya ya Longido pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya mheshimiwa mkuu wa mkoa amewapongeza viongozi hao kwa kusimamia vema utekelezwaji wa shughuli za maendeleo "Kweli kabisa na kwa dhati niwapongeze sana viongozi wa Wilaya hii kwa kuwa mmeamka sasa kazi inaonekana Niwaombe tusimamie na tuongeze nguvu kwenye usimamizi wa miradi ili ikamilike kwa wakati, hakuna kipindi ambacho Serikali imetoa pesa nyingi kama wakati huu hivyo basi tumsaidie Mheshimiwa Rais kutekeleza ukamilishwaji wa miradi ndani ya wilaya"Alisema mheshimiwa Mongella.
Mheshimiwa mkuu wa mkoa amewaasa viongozi wasiogope kujifunza ili kufanya kazi iwe nyepesi, pia amewaomba kamati ya Siasa wilaya kuwa macho kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo ili kutimiliza ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imelenga kuleta Maendeleo kwa wananchi.
Mheshimiwa John Mongella na timu kutoka mkoani wametembelea miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi unaoendelea wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mfano ya Mkoa mradi uliopokea fedha taklibani Shilingi Bilioni tatu (3)ambao ukamilishwaji wa shule hiyo ya mfano itachukua zaidi ya wanafunzi 800.
Pia ametembelea na kujionea ujenzi wa uzio wa shule ya Sekondari Longido pamoja na bweni la wavulana ujenzi unaoendelea shuleni hapo.
Sambamba na hilo Mkuu Mkoa amepongeza kamati ya ujenzi kwa kushirikiana na kufanya kazi nzuri.
Pia Mheshimiwa alitembelea baadhi ya majengo ya Hospital ya Wilaya ambako mbali na kupongeza pia ameagiza marekebisho madogo madogo yafanyike pamoja na kuweka umeme wenye nguvu kwenye majengo yasio na umeme wenye nguvu ili wananchi waendelee kupatiwa huduma nzuri kwenye Hospital hiyo kwani vifaa vingi vipo hivyo basi hakuna sababu ya kuendelea kuchelewesha baadhi ya huduma kwa watanzania
"Tafadhali naomba mjitahidi sana kukamilisha kwa haraka ujenzi wa bweni hili la wavulana ili wanafunzi hawa waweze kuingia na kuendelea na masomo yao bila matatizo yoyote, ofisi yangu ya mkoa itaunga mkono kwa kutoa bati 100 pamoja na mifuko ya sement 50 ofisi ya mkuu wa Wilaya itoe bati 50 na wazazi bati 100 sioni sababu ya ucheleweshaji wa ujenzi wa bweni hili "Alisema Mkuu wa Mkoa alupotembelea ujenzi wa bweni la wavulana shule ya Sekondari Ketumbeine unaojengwa kwa fedha za TASAF ambao serekali imetoa kiasi cha Shilingi Milion 155 na bweni hilo linataraji kuchukua zaidi ya wanafunzi 80.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Longido mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi amemshukuru Mkuu wa Mkoa na wajumbe aliofuata nao kwa kutembelea na kujionea utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo Wilayani humo. Mkuu wa Wilaya ameishukuru sana Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa pesa nyingi na kuwekeza kwenye miradi hii ya maendeleo Wilayani kwake, Mheshimiwa Ng'umbi ameahidi kuisimamia miradi yote kwa kushirikiana na viongozi wote waliopo Wilayani humo pamoja na wananchi ili waweze kujua nini serikali inafanya kwenye jamii yao"Mheshimiwa mkuu wa Mkoa sisi Longido tumejipanga vizuri sana kumsaidia Rais kwenye usimamizi na utekelezaji wa miradi kwenye Afya, Elimu maji na hata miundo mbinu ya barabara na Madaraja ". Alisema Mheshimiwa Ng'umbi
Nae Mzee Thobiko ambae ni mkazi wa kijiji cha Longido amemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na wajumbe kwa kutembelea miradi ya maendelaeo," Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutupendelea Longido na kutupatia fedha nyingi , tunashukuru Mkuu wa Mkoa kwa kufika na kutembelea miradi tunayofuraha sana na tunamkaribisha sana Longido," Alisema mzee huyo.
Ziara ya mkuu wa Mkoa Wilayani Longido ni ya siku mbili ambapo tarehe 8/11/2023 Mheshimiwa atakamilisha ziara yake kwenye miradi ya maendeleo Wilayani humo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Mheshimiwa Mongella alipo kuwa akikagua moja ya majengo ya Hospital ya Wilaya
Mh. Mongella kwemye ujenzi wa bweni la wavulana Longido Sekondari.
Mkuu
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM