Mkuu wa wilaya ya longido ndg. Daniel G. Chongolo amezindua rasmi bodi ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya longido mkoani Arusha leo tarehe 07/02/2018.
Wakati akizindua bodi hiyo ndg. Daniel ameeleza kuwa changamoto kubwa inayoikumba zoezi la utoaji wa huduma ya afya ni mifumo na miundo mbinu inayotumika katika utoaji wa huduma hiyo, huku akifafanua zaidi kuwa wilaya ya longido ina tarafa nne na vituo vitatu vya afya viwili vya serikali na kimoja cha binafsi hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa kuongeza vituo vya afya ili kukidhi mahitaji ya watu.
Vilevile mratibu wa bodi ya afya Dr. Justice E. Munisi ameeleza kuwa kwa upande wao wamejitahidi kutoa huduma mbalimbali kama mafunzo ya kudhibiti ukimwi, kutoa chanjo, uzazi wa mpango , mama na mtoto lakini wamefanikiwa kwa asilimia ndogo kutokana na changamoto zifuatazo;1. usafiri 2.kuhama hama kwa wagonjwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine hivyo kuonekana kwa idadi kubwa ya wagonjwa watoro 3. Umbali kati ya kituo cha afya na walengwa.
Hivyo basi mwenyekiti wa bodi ya afya ndg. Isack Ole ndetero ameahidi bodi hiyo kuwa bega kwa bega wakishirikiana na kuhakikisha kukaa vikao kwa muda na kutekeleza mipango kwa wakati ili kutimiza malengo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM