Wananchi wa Longido na wa nje ya Halmashauri ya Longido wamenufaika kwa kununua magari, Mitambo chakavu na Pikipiki katika mnada uliofanyika leo tarehe 03/04/2019 katika makao makuu ya Halmashauri .
Mnada huo uliendeshwa na Wakala wa Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA-ARUSHA) kwa kushirikiana na muuza mali(dalali) kutoka TRA.Mali zilizouzwa ni magari 2 ,trekta 1 ,tela la trekta 1 na pikipiki 4.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndg Jumaa Mhina amesema Mnada huu ni wa siku mbili na kesho tarehe 04/03/2019 mnada utaendelea tena kwa kuuza magari na mitambo iliyopo katika karakana ya Wakala Ufundi na Umeme Serikalini (TEMESA-ARUSHA) na Lolkisale Monduli.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM