Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameipongeza halmashauri ya Longido Mkoa wa Arusha Kwa usimamizi mzuri wa fedha za UVIKO 19 walizopatiwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi kwenye hospital ya wilaya(ICU).
JENGO LA ICU -HOSPITALI YA WILAYA
Alisema serikali imejenga majengo Kama hayo 25 nchi nzima kwenye hospital za wilaya na 75 katika vituo vya afya,aidha alieleza kuwa ujenzi wa majengo hayo utasaidia kuokoa maisha ya wannachi kwa kuwa huduma imesogezwa karibu.
Alisema hayo katika ziara ya kikazi alipotembelea jengo Hilo la ICU Lenye thamani ya Sh.million 250 na kukagua mradi wa maji kimoukwa _Namanga uliogharimu zaidi ya sh.Bilion 6,na kueleza kuwa wananchi wa mji wa Namanga walikua wakiteseka kwa miaka mingi bila maji safi na salama lakini serikali imetambua changamoto hiyo na kuchukua hatua.
TANKI LA MAJI KIMOKOUWA
"Hapa ni lango la biashara Kati ya Kenya na Tanzania,fanyeni biashara zenu kwa Amani mradi huu ni endelevu na mtanufaika nao zaidi,nimeambiwa hapa maji yanapatikana zaidi ya Lita million 4 ni mengi" alisema Msigwa.
Miradi iliyotembelea ni Mradi wa Maji Tanki la Kimokouwa,Kiwanda Cha nyama Cha Elia food overseas ambacho kinanifaika na mradi huo mkubwa wa maji kutoka siha mkoani Kilimanjaro wenye kilomita zaidi ya 75 ,mradi wa maji Namanga pamoja na ujenzi wa jengo la ICU hospital ya wilaya ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM