WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF ADOLF MKENDA AWATAKA WANAFINZI WA KIDATO CHA SITA NA WAMILIKI WA SHULE KUTOFANYA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA INAYOTARAJIA KUANZA 02/05/2023.,
Mh.Prof MKENDA ameyasema hayo Leo tarehe 29/04/2023 katika Mahafali ya kidaato Cha sita katika shule ya sekondari Longido iliyopo Wilayani Longido,
"Msingatie masharti ya mitihani,wale wote wasioandika majibu,matokeo yao yatafutwa na usiingie kwenye chumba Cha mtihani na kitu chochote,na shule zote zitakazo ratibu wizi wa mitihani iwe maafisa wa serikali au wamiliki wa shule watasababisha shule hiyo kufungiwa kuwa kituo Cha mitihani Kwa kuanzia na tukijiridhisha ni utamaduni shule hiyo itafutwa na nitoe tahadhari katika mitihani itayoanza tarehe 02/05/2023 tumejipanga kupata taarifa kila Kona ya nchi hii," alisema Mh.Prof mkenda.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM