Katibu tawala Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kiamia leo tarehe 07-10-2021 amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Longido na kuongea na watumishi katika ukumbi wa Halmashauri na kuwataka watumishi wa Halmashauri ya Longido kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kupunguza malalamiko yanayojitokeza katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali na kupunguza uonevu kwa watumishi
Alisema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kukumbushana wajibu wa utendaji kazi na kupokea malalamiko au changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Dkt Kiamia akizungumza Hali ya ukusanyaji wa mapato alisema wilaya hiyo bado Kuna Wigo mdogo wa ukusanyaji wa mapato na usiposimamiwa vizuri miradi ya maendeleo itashindwa kutekelezwa ipasavyo na kwa wakati.
Akifafanua juu ya fedha za makusanyo ya mapato ya ndani alisema fedha hizo ni za serikali kuu hazina tofauti na fedha za Ruzuku,na kuitaka halmashauri kutenga asilimia 40 ya mapato ya ndani kila mwezi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.
" Kwenye hiyo asilimia 40 ndani yake Kuna asilimia 10 ya makundi maalum ambayo ni Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu,Na fedha hizi zisipotolewa kwa makundi hayo tutahitaji maelezo" alisema Dkt Kiamia.
Katika hatua nyingine alisema utaratibu wa kubadili matumizi ya fedha Kama ilivyoelekezwa ni lazima kuandika barua kuomba kubadili matumizi bila ridhaa ni kosa na ulinganishwa na ubadhirifu wa fedha za Umma,hivyo aliwataka idara ya Mipango kusimamia vyema miradi ya maendeleo katika ngazi zote.
Hata hivyo alitoa agizo kwa wakusanyaji wa ushuru wanaodaiwa na halmashauri hiyo kuhakikisha wanarejesha fedha hizo haraka siku ya leo na kuwachukulia hatua wakusanya mapato wote wanaodaiwa fedha hizo.
" Nitawachukulia hatua,hapa Nimeona wanaodaiwa ni watu 27 nilishatoa maelekezo awali naona hayajatekelezwa , viongozi wakuu wa serikali akiwemo Waziri Mkuu anakemea ubadhirifu huu wa fedha za Umma ambao pia ni agizo la Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu" alisema Dkt Kiamia.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Stephen Ulaya alisema kuna baadhi ya wakusanya ushuru wadaiwa na wanaendelea kuzifuatilia kwa ukaribu sana ili ziweze kurejeshwa.
Naye Mwanasheria wa Halmashauri Erick Justine alisema " Mh RAS tumechukua hatua na tunaendelea kuhakikisha fedha zinarejeshwa pia tumepokea ushauri wako wa kufanya kazi kwa taratibu na kuafuata miongozo ya serikali" alisema Justine
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM