Mkuu wa Mkoa Arusha Mheshimwa John Mongella ameendelea na ziara yake Wilayani Longido ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Wilayani humo iliyoanza tarehe 7/11na kukamilika tarehe 8/11.
Mkuu wa Mkoa ametembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya Mundarara, amewataka viongozi wa wilaya kufanya hima na jitihada za kukamilisha mradi huo ili wanafunzi waweze kuanza masomo na kuyatumia majengo hayo.
Mheshimiwa ametembelea mradi wa ujenzi ya Kituo cha Afya Leremeta kilichopo kwenye Kata ya Sinya Wilayani Longido,
Akizungumza na wakazi wa kata hiyo Mheshimwa Mkuu wa Mkoa ametoa salamu zake za dhati kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa amewaona na amesikia kilio chao na yuko tayari kutatua matatizo yao ikiwemo Zahanati shule, miundo mbinu kama barabara, madaraja.
Pia Mkuu wa Mkoa amemuagiza Kaimu Mganga Mkuu Daktari Matthew Majani kukamilisha mradi huo ifikapo tarehe 8/12/2023, Sambamba na kupeleka wahudumu katika kituo hicho.
Vile vile ametoa pongezi kwa wananchi wa kata ya Kamwanga alipotembelea ujenzi wa shule kwa Mradi wa Boost ambao umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 112 ujenzi wa shule mpya ya Kamwanga kwa Mradi wa SEQUIP ambao Serikali imetoa jumla ya shilingi Milioni 500, ujenzi wa shule mpya ya Irkaswa mradi unazaidi ya milioni 600, pamoja na madarasa ya awali shule ya Irkaswa.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameitaka jamii kufahamu miradi mbali mbali inayofanyika kwenye jamii yao na kuchangia kuitunza na kutoa michango yao pale inapohitajika kwenye ukamilishaji.
"Niwapongeze sana watu wa Kamwanga kwa kuonesha mna muamko mkubwa sana juu ya mambo yanayoendelea katika nchi yetu hasa kwa hizi pesa nyingi zinazotolewa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yale yanayowastaili zikiwemo shule ambazo zitasaidia sana watoto kutotembea umbali mrefu kufuata shule ilipo, ujenzi wa shule hii mpya ya Kata ya Kamwanga ambayo Serikali imetoa zaidi ya milioni 500 kutekeleza mradi huo".Alisema Mkuu wa Mkoa.
Nao wakazi wa Kamwanga wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea maendeleo makubwa kwenye kata yao"Tunamshuru sana Rais kwa kutukumbuka mana sasa tunayo maji, tunazahanati japo bado zinachangamoto, tuna umeme, japo haujafika kwenye vijiji vyote, tuna barabara amabayo tunaomba utekelezaji wa barabara ya Longido-Kamwanga-hadi Rombo Tarakea ili itusaidie kwa shughuli mbali mbali"Alisema ndugu Sara Lemayani mkazi wa Irakaswa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Longido mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi amemshukuru sana Mheshimwa Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi hiyo ya shule Zahanati na Barabara, pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuja na kukagua miradi hiyo ya maendeleo kwa ziara hii inasaidia sana kuhimiza ukamilishwaji wa miradi. Sambamba na hilo Mheshimiwa Ng'umbi amewashukuru sana wananchi wa Kamwanga kwa nguvu kazi na michango yao katika kuleta Maendeleo kwenye kata yao."Niwashukuru sana watu wa Kamwanga kwa kujitoa kwenu na utulivu wenu katika kutekeleza na kukamilisha miradi hii"Alisema Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Ziara hizi za mkuu wa Mkoa kwenye miradi ya maendeleo ni ziara endelevu ambazo zinafanyika mara kwa mara kutimiza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye kuleta Maendeleo ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM