Maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani kitaifa yamefanyika Mei 5, 2019 katika Uwanja wa Bariadi Mkoani Simiyu ambapo mgeni rasmi alikuawa ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile aliyemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Awali Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa waandishi wa habari ofisini kwake amewakaribisha wakunga wote nchini na kuwaakikishia mkoa umefanya maandalizi ya kutosha.
Makamu mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini Dkt. Hashina Begum amesema kuwa kauli mbiu ya siku ya Wakunga duniani 2019 “Wakunga ni watetezi wa haki za wanawake” inakumbusha umuhimu wa Wakunga katika kuwatetea akina Mama wakati wa uja uzito, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Vilevile Begum amebainisha kuwa UNFPA imeendelea kushirikiana na serikali katika ukarabati wa vituo 38 vya Afya, Wodi za wazazi na vyumba vya upasuaji, ununuzi wa vifaa na mashine za kumwezesha mkunga kutoa huduma ya mama na motto kwa urahisi na kuwajengea uwezo wakunga 90 kutoka vituo vilivyokarabatiwa kutoa huduma za daraura kwa mama na motto.
Naye Rais wa Wakunga Tanzania (TAMA) Feddy Mwanga amesema TAMA inafanya kazi Mkoa wa Simiyu toka mwaka 2016 kwa kuwaelimisha wakunga ili waweze kutoa huduma za dharura kwa mama na mototo hususani katika vituo vya pembezoni, huku akishukuru UNFPA kwa mchango wake kifedha na utaalamu kuwezesha mafunzo hayo,
Amehitimisha kwa kusema kuwa dira ya TAMA ni kuona kuwa kila mama mjamzito anayejifungua na watoto wachanga wanapata huduma bora.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM