Halmashauri ya Wilaya ya Longido imeendelea kujidhatiti katika kuhakikisha inaboresha vitendea kazi vya ukusaji wa mapato ikiwa pamoja na kuwatembelea mara kwa mara wahusika wa mapato kazini kwao ili kama kuna changamoto zitatuliwe haraka.
Mapema leo julai 5, 2019 Afisa Tehama Wilaya Bi. Zainabu Mzee amewatembelea wakusanyaji wa ushuru mbalimbali hususani katika Mipaka ya Namanga (Border Cross Fee) soko la mifugo ya Eworendeke na wakusanya ushuru wa Mazao Longido ili kukagua kama Mashine zote zinafanya kazi ipasavyo na ziko hewani(online) sambamba na kuwapatia Vitamblisho vyenye majina halisi ya mkusanyaji ili kuwatambua kwa majina na sura na kuwaagiza kuvivaa shingoni muda wote.
Aidha Afisa TEHAMA Zainabu amewaasa wakusanya ushuru kuhakikisha wanatunza mashine hizo kwa uangalifu na kutozichanganya kwa namna yeyote ile kwani kila mkusanyaji amepewa mashine yake mwenyewe yenye laini lakini ineorodhesha aina za mazao ama bidhaa zinazotakiwa kutozwa ushuru.
Awali wakati akitoa vitambulisho kwa wakusanyaji wa ushuru katika mipaka ya Namanga maeneo mbalimbali kama machinjio ya nyama amewataka kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu kulingana na utaratibu wanaoelekezwa bila kuzichezea mashine wala kufanya kazi offline.. Vilevile ameendelea kuwasisitiza kuvaa vitambulisho muda wote ili mtu kutambua haraka nani na anatoka wapi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM