Ziara ya ukaguzi wa miradi ya inayotekelezwa chini ya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi imefanywa na wataalam kutoka ngazi ya taifa ,mkoa ,wilaya katika wilaya ya longido leo tarehe 18/01/2018.
Mratibu wa miradi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi ndg.Ally msangi na mhandisi Evarist Lelo wametoa ufafanuzi kuhusiana na miradi hiyo kuwa katika wilaya ya longido kwa sasa kuna miradi 14 inayoendelea kutekelezwa chini ya miradi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi itakayo gharimu tshs.805,782,499.43 ikiwa ni gharama ya ujenzi na 727,243,499.43,usimamizi wa miradi wakati wa utekelezaji 41,598,000na mafunzo kwa kamati za kusimamaia miradi baada ya kukamilika 27,273,500 na ununuzi wa vifaa na madawa 21,585,000.
Vilevile wameorodhesha miradi hiyo kama ifuatavyo 1; miradi ya maji katika vijiji vya Alaililai,Orbomba,Namanga, Kiserian na Eorendeke na kati ya miradi hiyo iliyoko Eorendeke, Alaililai,Orbomba imekamilikan na Namanga na Kiserian iko katika hatua ya mwisho kukamilika 2;mradi wa kununua vifaa na kukarabati kituo cha afya cha mifugo Tarafa ya Engarenaibor,3; miradi miwili ya ukarabati wa maji katika vijiji vya Matale'A' na Losirwa ipo katika hatua ya mwisho kukamilika, 4;Mradi wa kuhifadhi chanzo cha maji katika kijiji cha Mairouwa ,5; Miradi miwili ya kujenga vibanio vya mifugo vijiji vya Irkaswa na Olmolog na kukarabati Josho Moja katika kijiji cha Lerangwa na 6; miradi miwili ya maghala katika vijiji vya Ildonyo na Mairouwa.
Pia kiongozi wa msafara huo kutoka ofisi ya katibu mkuu wa TAMISEMI Dr.komba ngazi ya Taifa amewasisitiza wananchi kwa ujumla kwamba pamoja na kuwa ujenzi wa miradi hiyo inaendelea kutekelezwa ni wajibu kila mmoja kuitunza miradi hiyo ili iweendeleza na kutumiwa na kizazi kijacho na kuwa taka wahandisi wate wanaohusika na shughuli hiyo ya ujenzi wawe makini na kuhakikisha miradi inakamilika kwa muda mwafaka kwani tofauti na hapo hakuna malipo yoyote itafanyika kwa atakaye vuka muda wa makubaliano ya mikataba iliyosainiwa.
Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya mabadiliko ya hali hewa na tabia ya nchi ndg.Michael Saytoti ameweza kuaandaa taarifa ya kila mradi ambapo imeeleza changamoto , manufaa na wanufaika wa miradi hiyo kuwa changamoto kubwa ni uhaba wa maji hali inayosababisha ukame na kudidimia kwa uchumi na hata magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji hivyo manufaa ya miradi hiyo nikuwa inua kiuchumi,kimaendeleo na kupungua kwa magonjwa ya mlipuko na ya mifugo na kupungua kwa hali ya ukame na njaa kutokana na uhifadhi wa chakula kipindi cha mavuno na kutumika kipindi cha njaa.
Hivyo basi mkuu wa wilaya ya longido ndg.Daniel G. Chongolo na kaimu mkurungenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido ndg.Geryson mtera wameshukuru sana kwa ziara hiyo fupi iliyofanyika ndani ya wilaya ya longido huku wakiwaomba wataalamu hao wasisite kuwaambia mapungufu watakayoyaona katika miradi hiyo na kuwaahidi kuwa ndani ya siku 14 zijazo watakuwa wamekamilisha miradi hiyo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM