Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na katibu tawala wilaya Khamana Simba wamekagua miradi iliyokuwa ikitekelezwa katika Ikolojia ya Ziwa Natron na Shirika la Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) kwa kushirikiana na Mfuko wa hifadhi wanyamapori (WWF) kwa fedha za ufadhili wa serikali ya Ujerumani (BMZ).
Katika ziara hiyo,Simba aliwashukuru wadau hao kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na kuwaomba wasiishie hapo bali wawafikie na wakazi wengine katika Ikolojia ya Ziwa Natron.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: +255 272 970 793/ 94
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.