Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi amefungua rasmi kikao cha maelekezo ya utekelezaji wa mradi wa Boost unaofadhiliwa na Bank kuu ya Dunia leo tarehe 9 may 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido
Akitoa maelekezo hayo ya utekelezaji wa mradi huo wa Boost wa P4R (PAY FOR RESULTS) Mkuu wa wilaya amewataka wasimamizi wa mradi pamoja na walimu wa kuu walionufaika na mradi huo wa ujenzi wa shule za msingi pamoja na madarasa ya awali kuwa makini kwenye usimamizi wa mradi ili kupata majengo mazuri na viwango vya hali ya juu kwa kuwa mradi huu ni walipa kwa matokeo ili tuweze kupata fedha nyingine za kuendeleza mradi na miradi mingine mingi inayokusudiwa ndani na nje ya Halmashauri
"Sitegemei kuona tunashindwa kwenye kutekeleza mradi kwa namna yeyote ile maana hatuna sababu ya kushindwa"alisema Mheshimiwa Ng'umbi
Mheshimiwa Ng'umbi amewataka wasimamizi wa mradi huo kuwashirikisha kwa karibu wananchi ama jamii nufaika wa mradi ili kuwafanya wawe sehemu ya mradi kwani wanaweza kusaidia kwenye shughuli za kawaida za utekelezaji kama kusogeza mawe kuchimba msingi, pamoja na shughuli nyingine ndogo ndogo
Pia amesisitiza sana kufuata taratibu zote za manunuzi, bidhaa zinunuliwe kihalali kwa utaratibu uliowekwa "Msithubutu kununua bidhaa kwa wazabuni mana hatutapata bidhaa bora na kwa bei nafuu" Alisema Mheshimiwa Ng'umbi
Sambamba na hilo ameomba mikataba ya mafundi kufuata taratibu na lazima ipitiwe na mwanasheria ili kudhibitisha ubora, ufanisi na uwezo wa kazi zake.
Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Longido ndugu Stephen A Ulaya ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa jitahada zake za kuboresha elimu katika shule za msingi sambamba na ujenzi na uboreshwaji wa madarasa ya awali na ameahidi kusimamia mradi huo kwa karibu zaidi ili kurahisisha ufanisi wake.
"Mheshimiwa mkuu wa wilaya kwa niaba ya walimu wakuu wanufaika wa mradi tunaahidi kusimamia kazi hii kwa umakini na weledi wa hali ya juu ili tuweze kupata miradi mingi na yenye tija kwa wanachi wetu"Alisema Mwalimu Deusdedit Afisa Elimu Msingi halmashauri ya wilaya ya Longido.
*Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM