Halmashauri ya Wilaya ya Longido chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ngd. Jumaa Mhina kupitia Idara ya Afya wameendelea kushirikiana vyema na wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa kwa kuahakikisha wanapunguza na hata kumaliza kabisa vifo vya Uzazi wa akina Mama na watoto.
Akifungua kikao cha kampeini yenye kauli mbiu isemayo “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” na maneno ya “Maneno sasa basi, Vitendo tu! Jiongeze! Tuwavushe salama. Mama mjamzito akivuka salama Mtoto atakuwa salama, Familia itavuka salama na Nchi itakuwa salama” Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank James Mwaisumbe asubuhi ya Juni 20,2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Longido amesema kuwa vifo vya uzazi wa akina Mama na watoto vinaweza kuisha kabisa kama tu wahusika wote watawajibika ipasavyo.
Aidha Mhe. Mwaisumbe ameeleza kuwa Serikali inatambua uwepo wa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya Afya ikiwemo Vituo vya Afya, barabara, magari, maji n.k na ndio maana imekwishaanza kuchukua hatua za haraka kwa kuwajengea kituo kikubwa cha Afya ambayo ni Hospitali ya Wilaya na inatarajiwa kukabidhiwa mwishoni mwa mwezi juni, kuwaletea mradi mkubwa wa maji ambao umekwishaanza kusambaza maji ndani ya Longido pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara na umeme.
Mapema kabla ya ufunguzi wa kampeini hiyo Mkurugenzi mtendaji Ndg.Jumaa Mhina amesema kuwa Longido sasa ni kitovu cha maendeleo kwani ni miongoni mwa Wilaya ambazo zinaendelea kupewa kipaumbele na Serikali ya Dk. John Magufuli kwa kuboresha miundombinu.
Naye mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk.Wedson Sichwalwe amefafanua jitihada za maksudi za Kupunguza na kumaliza kabisa vifo hivyo zinaonekana kwani kipindi cha Januari-Machi 2019 akijatokea kifo chochote cha uzazi wa Mama na Mtoto katika Mkoa wa Arusha.
Justice Eliangao Munisi Mganga mkuu wa wa Wilaya Longido amema kuwa kupungua kwa vifo hivyo kumechangiwa na kampeini za mara kwa mara za kuongeza uwajibikaji wa wataalamu katika kuzuia vifa vya Mama na Watoto.
Hata hivyo amebainisha kuwa zipo changamoto kama ubovu wa miundombinu, ukosefu wa magari ya wagonjwa,wazazi kutokwenda ama kuchelewa kufika kujifungulia katika vituo vya Afya. Vilevile amesema kuwa njia zitakazoendelea kusaidia kutatua vifo hivyo ni pamoja na dawa za kuzuia kifua cha mimba,wataalamu kutoa mabaka ya uzazi pamoja na kusaidia mtoto mchanga ambaye hana nguvu mara baada ya kuzaliwa.
Katibu wa Afya Wilaya ya Longido Josia Mruve amesema sasa Longido imepiga hatua kubwa katika kutoa Elimu kwa wananchi kwani kwa mwaka 2017 akina Mama waliojifungulia kituo cha Afya ni 21% na katika kipindi cha Januari- Mach 2019 waliojifungulia katika vituo vya Afya ni 51%.
Kikao hicho kimehhudhuliwa na Wataalamu wa Afya kutoka Mkoani Arusha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido …………………………….,wanaharakati wa Afya Wilaya ya Longido pamoja na viongozi wa kimila.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM