Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank James Mwaisumbe amewata Vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujitolea wafanye vyema huko waendako ili kuonesha kuwa walistahili kuchaguliwa kwa kuwa Wilaya imefuata vigezo na masharti vilivyotanja katika Tangazo.
Mhe.Mwaisumbe ameyasema hayo jioni ya leo juni 19,2019 katika viwanja vya makao makuu ya Wilaya hiyo wakati akizungumza na Vijana wa Darasa la Saba, Kidato cha nne, Kidato cha sita pamoja na wenye Elimu ya juu, mala baada ya kufanya usahili na kuwachagua vijana stahiki kulingana na sifa zilizokuwa zimetajwa.
Amesema kuwa vijana kama walivyojitokeza kwa wingi ndivyo wanatakiwa kulitumikia Taifa ipasavyo na si kujihusisha na vitendo viovu pale wanapopewa nafasi za kiutawala “huko muendako hakikisha mnaendena na matakwa ya kijeshi na si kuiba, kutoa na kupokea rushwa,kuwa watekaji wala kujihusisha kwa namna yeyote hile katika vitendo viovu” Mhe. Mwaisumbe
Hata hivyo amewaomba maafisa wa jeshi la polisi kuwasajili vijana waliokosa sifa katika Jeshi la akiba yaani Mgambo ili na wao wajione wapo sehemu ya kulitumikia Taifa la Tanzania na wahesabike katika moja ya Majeshi ndani ya nchi yao.
Aidha amewatoa wasiwasi vijana waliokosa sifa kwa kuwahimiza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ile hali ya kuwa ndani ya Chama hicho kuna Fursa nyingi kuliko zilizopo Jeshini “nawasihi mistake tamaa kwa kukosa nafasi hii bado nafasi mnayo watakaoshindwa kujiunga na Jeshi la akiba nenda katika Ofisi za CCM mkajisajili ili muwe wanachama, katika CCM kuna fursa nyingi zaidi “ Mhe. Mwaisumbe
Usahili huo umeudhuliwa na Maafisa usalama wote wa Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurungenza wa Halmashauri ya Longido Ndg. Jumaa Mhina.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM