Halmashauri ya Wilaya ya Longido leo tarehe 31/05/2022 imetoa mkopo usio na riba wa shilingi milioni mia moja(100.000,000/-) kwa vikundi 17 vya Wanawake,Vijana na Wenye Ulemavu.Akikabidhi Hundi hizo Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh.Nurdini Babu ameagiza vikundi vyote vilivyopatiwa mikopo na kushindwa kurejesha anavipa muda wa Mwezi mmoja kurejesha fedha hizo kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao. Mh.Babu amesema marejesho hayo ya mikopo itasaidia vikundi vingine kupatiwa mikopo hii.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Simon Oitesoi amevitaka vikundi hivyo vilivyopatiwa mikopo kuwa mabalozi wazuri kwa kuhimiza ulipaji wa mapato ya Halmashauri kwani mikopo hiyo waliyopatiwa inatokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na tunatekeleza ILANI ya Chama cha Mapinduzi kwa kutoa mikopo katika kila robo ya Mwaka..
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg.Steven Ulaya amesema ni takwa la kisheria kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Wenye Ulemavu,Na kwa sasa serikali inataka pesa hizi zitolewe kwa vikundi vichache vyenye tija na safari hii kwa mara ya kwanza tumetoa milioni 20 kwa kikundi kimoja cha Wanawake,Pia Ulaya amesema ucheleweshwaji wa marejesho ya Mikopo inasababisha Halmashauri kupata hoja za ukaguzi za CAG..
Vile vile Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi Grace Mghase amesema vikundi viliivyopatiwa mkopo ni vikundi vya Wanawake 7,Vijana 9 na watu wenye ulemavu kikundi kimoja. na Kikundi cha Wanawake kimepatiwa shilingi 57,000,000/-,Vijana Sh.45,000,000/- na Walemavu Sh.4,000,000/-.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM