Mkuu wa wilaya ya Longido Mh. Frank James Mwaisumbe wakishirikiana na jeshi la polisi la mpakani leo tarehe 26/06/2019 wamefanikiwa kuwatia mbaroni vijana wawili wa wakitanzania wakijaribu kutorosha madini ya aina mbalimbali yenye jumla ya kilogram 36.5 za madini, madini hayo ikiwemo kilo 24.2 za tanzanite kilo 3 za ruby kilo 3 za green granite na kilo 5.9 za aina nyingine za madini ambayo haikujulikana kuwa ni aina gani.
Akizungumza katika tukio hilo Mh mkuu wa wilaya alisema jeshi la polisi walipo kuwa wakifanya ukaguzi wa kawaida wa magari ya mizigo ndipo walipopata shaka na gari lililokuwa limebeba mchele na kuamua kufanya upekuzi wa kina kwa kutumia mbwa wa jeshi la polisi na kufanikiwa kukamata mfuko wenye madini hayo uliopangwa sawa na mifuko ya mchele ambayo bado dhamani yake haijulikani .
Vijana hao walisema wameagizwa kupeleka madini hayo kwa mtu ambaye atatumiwa namba yake ya simu watakapofikisha mzigo ili awapokee Mpakani mwa Tanzania na Kenya mpaka wa Namanga
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameamuru mzigo huo upelekwa ofisi ya madini ili kubaini dhamani yake.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amewatahadharisha wafanya biashara wanaohujumu uchumi na kuwaambia Longido sio uchochoro wa kupitisha mali za nchi yetu na kukwepeshe serikali mapato halali sisi na jeshi letu tumejipanga kuhakikisha kuwa hakuna chochote kitakacho pita hapa bila kulipa kodi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM