Halmasahauri ya wailaya ya Longido Leo tarehe 24/11/2022 imetekeleza agizo la Serikali ya awamu ya sita la kuwataka watoto wote kaunzia miaka mitano hadi kumi na nne wanapewa dawa aina ya Albendazole kwa ajili ya kuzuia minyoo ya tumbo amabayo imekuwa tishio kwa watoto wengi nchini Mkurugenzi wa halamsahauri ya wilaya ya Longido ndugu Stephen Ulaya alifungua mafunzo ya utekelezaji wa zoezi hilo mnao tarehe 23 Novemba kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido na baadae zoezi la utekelezaji wa ugawaji wa dawa za kudhibiti minyoo kufanyika katika shule zote za msingi zilizopo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Longido ambako takribani watoto wote wenye umri kuanzi miaka mitano hadi kumi na nne wamepatiwa dawa hizo ili kuzuia magonjwa yote yanayotokana na minyoo ya tumbo
Zoezi hili ambalo limekuwa likifanyika mara kwa mara likiwa limelenga hasa kuondoa na kuthibiti magonjwa mbali mbali yanayotokana na minyoo ya tumbo ambayo yamekuwa yakileta madhara makubwa hasa kwa ukuaji wa mtoto pamoja na kumfanya mtoto kupoteza hamu ya kula kupungua uzito hususani na kuvimba sehem mbali mbali ya mwili hususani tumbo baadae kupelekea hata magonjwa ya ini na mengineyo
Nae Dr Selemani Mtenjela mkuu wa kitengo cha Afya, Lishe na Ustawi wa jamii amewaomba wazazi kutokuwa na imani potofu juu ya dawa hizo na kuwataka wazazi wawaruhusu watoto kupewa dawa hizo kwa ajili ya kuimarisha Afya zao, Dr Selemani amesema dawa hizi ni salama na ni maalumu kwa ajili ya kuthibiti magonjwa yatokanayo ma minyoo ya tumbo
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM