Waziri wa uchukuzi Prof.Makame Mbarawa leo tarehe 05/06/2022 amefungia mizani ya kisasa ya Kimokouwa uliopo Wilayani Longido ambayo itatumika kupima uzito wa magari yanayofanya safari zake kati ya Tanzania na nchi jirani ya Kenya..
Mh. Waziri amewataka wazimamizi wa mizani hiyo inayosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini(TANROADS), Kutenda haki kwa wasafirishaji hasa wanapokuwa na makosa ya kuzidisha uzito.
'Sheria inayosimamia mizani ya Afrika Mashariki ni kali sana na ina tozo kubwa hivyo hakikisheni mizani inakuwa katika vipimo sahihi ili kuondoa mkanganyiko wa uwiano wa mizani unaojitokeza mara kwa mara" amesema Prof.Mbarawa..
Aidha ,Prof. Mbarawa amekemea vitendo vya vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa mizani kwani athari ya kumuandikia msafirishaji tozo ni kubwa na nyingine zainagharimu zaidi ya gharama ya gari husika.
'Angalieni namna bora ya kuelimisha kwani unakuta gharama ya tozo ni kubwa kuliko hata thamani ya gari husika na kwa mujibu sheria lazima itozwe tozo' amefafanua Prof Mbarawa.
Waziri Mbarawa ametoa agizo kwa TANROADS kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya mara kwa mara kwa watumishi wa mizani,wasafirishaji na madereva kuhusu sheria ya mizani pamoja na kufanya tafiti kujua tatizo la kutokuwa na uwiano sawa wa uzito wa gari kutoka mzani mmoja hadi mwingine.
Pia Prof. Mbarawa amewahaidi Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha Taa za barabarani.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM