"HODI LONGIDO NIMEKUJA KUWAONA, NIMEFURAHI KUWAONA" Ni maneno yake Mheshimiwa, Daktari Alice Kaijage, Mbunge wa wafanya kazi alipofanya ziara yake na kukutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido katika ukumbi wa J. K. Nyerere leo tarehe 24 /11 /2023. Akizungumza na watumishi Daktari Kaijage amewaasa wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi na jamii inayo wazunguka,sambamba na hilo Mheshimiwa ameiomba idara ya Utawala na Rasilimali Watu kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakuta watumishi kwenye maeneo yao ya kazi sambamba na stahiki zao kama kupanda kwa madaraja, upandishwaji wa vyeo,kuumia kazini na mambo mengi yanayofanana na hayo.
Mheshimiwa Mbunge ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Daktari Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatazama watumishi wa idara tofauti tofauti kwa jicho la upekee kwani katika miaka mitatu ya nafasi yake kama Rais watumishi zaidi ya 450,000 wamepanda madaraja, wengine wamelipwa stahiki zao za malimbikizo ya mishahara,posho za madaraka pia imetoa ajira kwa watumishi wakada mbalimbali za utumishi wa umma.
Nae Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Dominic Ruhamvya ameishukuru serikali ya awamu ya sita ndani ya miaka mitatu kwa kuwakumbuka watumishi wa umma kwa kuwapatia stahiki zao pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Clemence Kenyatta amemshukuru Mheshimiwa Alice kwa kuja kuzungumza na watumishi wa umma wa wilayani hapo, pia amemuomba Mheshimiwa Mbunge kufikisha baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo zikiwemo zile zinazohusiana na stahiki za watumishi, kutoa mafunzo kazini kwa Watumishi wa Serikali ili kuongezea ujuzi wawapo makazini, pamoja na kurudisha sera ya kuwaendeleza watumishi waliopo kazini.
"Asante sana Mheshimwa Kaijage kwa kuja kuzungumzia na sisi watumishi tuliopo Wilayani hapa tunaahidi kutekeleza yale yote uliyo tuagiza kama mlezi na msemaji wa watumishi bungeni tunaahidi kufanya kazi kwa bidii na kuwasaidia watumishi kupata haki na stahiki zao kwa mujibu wa sheria wanapokuwa kazini na hata wakati wanapostaafu"Alihitimiasha Ndugu Peter Matemba Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wilaya.
Ziara ya Mheshimiwa Mbunge Kaijage ni ya siku moja Wilayani humo ikiwa na lengo la kufika na kuzungumza na watumishi na wafanya kazi kwenye Halmasahauri zote Nchini.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee.
Imeandikwa na Happiness E. Nselu
Kaimu Afisa Mawasiliano Serikalini Wilaya.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM