Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu,Mh.Jenista Joakim Mhagama leo tarehe 22/11/2017 ametembelea mradi wa ujenzi wa mnada wa kimkakati wa mifugo katika kijiji cha Eworendeke ,
Akiongea na wananchi katika eneo la ujenzi wa mnada ,Mh.waziri amesema ameridhika na utekelezaji wa mradi huo na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Dr.John Pombe Magufuli inatoa Tsh.123,692,513.59/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa mnada huo.
Pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Ndg. Jumaa Mhina wakati wa Ziara hiyo amesema, mradi huo upo chini ya program ya Miundombinu ya masoko,Ongezeko la Thamani na Huduma za fedha vijijini((MIVARF).Gharama za mradi huu hadi kukamilika TSH.659,059,750/= kati ya hizo MIVARF imechangia asilimia 95% na Halmashauri asilimia 5%.
Pia ameongeza kwa Kusema mradi hukikamilika unatarajiwa kuwa na manufaa yafuatayo:_
-Kuongeza uzalishaji wa mifugo kutokana na uwepo wa soko la uhakika la mifugo
-Kuboresha na kuinua kipato cha Wananchi wa Longido.
-Ajira kwa Vijana na Wanawake
-Kuongeza mapato ya halmashauri.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM