ya wilaya ya longido mkoani Arusha imezindua zoezi kupiga chapa ng'ombe leo tarehe 05/01/2018 katika kata ya Orbomba wilayani longido.
Akizungumza na wananchi wa kata ya orbomba mkuu wa wilaya ya longido ndg.Daniel G.Chongolo amesema sababu za kuchapa ng'ombe hao ni kuepukana na usumbufu wa ng'ombe kutoka nje ya nchi kuingia nchini bila ruhusa,kujulikana kwa idadi ya mifugo hao ndani ya nchi,kuepuka/kurahisisha matibabu kwa ngombe pindi wanapougua magonjwa ,ubora wa mifugo hao kulinganisha na sehemu zingine.
Pia daktari wa mifugo ndg.Safan Kagoma amewasisitiza wananchi hao kuwa kwa yeyote ambaye hatajitokeza /kushirikiana kwa kuficha ng'ombe au kukwamisha zoezi hilo atakapogundulika atachukuliwa hatua za kisheria ,hivyo basi ni wajibu wa kila mmoja kutoa ng'ombe wake wote na kuwekwa chapa.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Orbomba ndg.Motika Kasosi amefurahia zoezi hilo kuzindiliwa katika kata yake kwani kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji wamewaelimisha wananchi hao kuhusiana na zoezi zima la uchapaji ng'ombe na hatimaye kuitikia kwa kukubaliana nalo.
Vilevile wameeleza changamoto walizokumbana nazo ni kuwa baadhi ya walengwa hao wamewahamisha mifugo yao kutokana na hali ya ukame hivyo kuwa na mifugo chache napia wengine kuwa na mashaka kuwa pindi watakapowatoa mifugo yao kuwekwa chapa watakuja kudaiwa kodi.
Hivyo basi ni imani yao viongozi hao kuwa itakapofikia tarehe 22/01/2018 zoezi hilo litakuwa limekamilika kwani ni agizo kutoka kwa Rais Dr.John Pombe Magufuli huku wakiendana na kauli ya hapa kazi tu ya serikali ya awamu ya tano.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM